“Maono ya Nguvu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.
Maono ya Nguvu
Picha kutoka maisha ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu na nguvu yetu.
Yesu Kristo alikuja duniani ili kukusaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Ni Yeye pekee angeweza kufanya hivi.
“Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
“Mimi ni njia,ukweli, na uzima: hakuna mtu ajae kwa Baba,bali kwa kupitia kwangu.”
Wale wote wanaoteseka kwa aina yoyote ya udhaifu wanapaswa kukumbuka kwamba Mwokozi wetu pia alipitia aina hiyo ya maumivu na kwamba kupitia Upatanisho Wake anampatia kila mmoja wetu nguvu ya kuvumilia.”
Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, “Mwokozi Wetu Ametufanyia Nini?,” mkutano mkuu wa Okt. 2021 (Ensign au Liahona, Nov. 2021, 77).
Nguvu za Yesu Kristo hukuponya, hukusaidia kubadilika na kukupa nguvu za kuvumilia majaribu.
“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
“Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
“Mwokozi anapenda kurejesha kile usichoweza kurejesha; Anapenda kuponya majeraha usiyoweza kuponya; Anapenda kurekebisha kile ambacho hakiwezi kurekebishika; Yeye anafidia yasiyo sawa yote yaliyoshurutishwa kwako; na anapenda kuponya kabisa hata mioyo iliyovunjika.”
Mzee Dale G. Renlund wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, Mkutano mkuu wa Apr.2020 (Ensign au Liahona, Mei 2020, 44).
“Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza.”
Jifunze kuhusu Yeye. Kuwa na imani katika Yeye. Mfuate Yeye. Nguvu zake zinaweza kuwa nawe kila wakati.
“Siwezi kufanya peke yangu, na sihitaji iwe hivyo, na sitaki kufanya hivyo. … Kuchagua kuunganishwa kwa Mwokozi wangu, Yesu Kristo, kupitia maagano niliyofanya na Mungu, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.’ [Wafilipi 4:13].”
Rais Camille N. Johnson, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi, mkutano mkuu wa Aprili 2023 (Ensign au Liahona, Mei 2023, 82).
“Yeye ni nuru, uzima, na tumaini la ulimwengu. Njia Yake ni njia ambayo inaelekeza kwenye furaha katika maisha haya na maisha ya milele katika ulimwengu ujao.” “Mungu ashukuriwe kwa ajili ya zawadi isiyolinganishwa ya Mwanaye mtukufu.”
“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume,” Gospel Library.
Angalia aplikesheni ya Gospel Living mwezi huu kwa kazi za ziada za sanaa na video kuhusu maisha ya Mwokozi.