Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Maandiko 12 Kwa ajili ya Wakati Unapohisi …
Machi 2024


“Maandiko 12 kwa ajili ya Wakati Unapohisi …,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024, ukurasa–ukurasa.

Nguvu kutoka kwenye Maandiko

Maandiko 12 Kwa ajili ya Wakati Unapohisi …

Maandiko yamejaa miongozo, bila kujali jinsi tunavyohisi.

Picha
msichana akisoma maandiko

Vielelezo na Toby Newsome

Miaka kadhaa iliyopita, Elisabeth A., 17, kutoka Arizona, Marekani, alianza kuwa na wasiwasi, na hali ilizidi kuwa mbaya. “Nilihisi hivyo siku nzima, kila siku,” alisema. “Ilikuwa ngumu kwangu kumaliza siku.”

Ili kupata faraja, Elisabeth aliamua kusoma maandiko kila usiku. Baada ya muda, alianza kuhisi furaha zaidi.

“Nilijua sikuwa peke yangu,” alisema. “Nilijua kwamba Mungu alinipenda na alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, ambaye alihisi maumivu yetu, maumivu ya moyo, huzuni na kukata tamaa. Kupitia maandiko, nina uhusiano wenye nguvu pamoja na Kristo na mtazamo mzuri kama huo juu ya maisha!”

Elisabeth alijifunza kwamba maandiko yamejaa mistari na hadithi kuhusu jinsi gani tumaini, amani na nguvu zinavyopatikana katika Yesu Kristo. Wengi wa mashujaa wetu wa maandiko tunaowapenda walikabiliwa na hali ngumu. Na katika kila hali, walipata tumaini, amani na nguvu walipomgeukia Yesu Kristo.

Kusoma maandiko kunaweza kusitatue yale unayopitia, lakini kweli zinazofundishwa katika maandiko zinaweza kukupa nguvu na ahueni. Hapa kuna maandiko machache unayoweza kutafuta ikiwa unahitaji wazo la kutia moyo kwako au rafiki. Je, unaweza kupata maandiko yako mwenyewe?

Kwa ajili ya wakati unapohisi …

Huzuni: Mafundisho na Maagano 68:6

Kwa hiyo, changamkeni, na msiogope, kwani Mimi Bwana nipo pamoja nanyi, na nitasimama karibu yenu.

Picha
kijana akiwa kwenye huzuni, na mawingu yakiwa juu yake

Kutotosheleza: Luka 12:6–7

Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.

Picha
msichana akionekana mwenye aibu

Aibu: Isaya 54:8

Kwa fadhili za milele nitakurehemu.

Picha
kijana akimdhihaki kijana mwingine, ambaye anaonekana na huzuni

Enye huzuni: Alma 26:27

Mvumilie mateso yenu kwa subira na nitawapatia mafanikio.

Picha
kijana akionekana kutokuwa na tumaini, huku ameshika mkono usoni

Bila Tumaini: Moroni 7:41

Mtakuwa na tumaini kupitia upatanisho wa Kristo na nguvu ya ufufuko wake.

Dhaifu: Etheri 12:27

Ikiwa wakijinyenyekeza mbele yangu, na kuwa na imani ndani yangu, ndipo nitafanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu kwao.

Picha
mvulana akionekana na wasiwasi

Wasiwasi: Mafundisho na Maagano 84:88

Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu.

Picha
msichana akilia

Kuumizwa: Zaburi 30:2

Ee Bwana, Mungu wangu, nilikulilia, nawe umeniponya.

Picha
mvulana akionekana mwenye woga

Kuogopa: Yoshua 1:9

Uwe hodari na moyo wa ushujaa … kwani Bwana Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako.

Picha
msichana akionekana mpweke na mwenye huzuni

Mpweke: Yohana 14:18

Sitawaacha ninyi yatima: Naja kwenu.

Picha
mvulana na msichana wakibishana

Hasira: Moroni 7:48

Ombeni kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, kwamba mjazwe na upendo huu.

Picha
msichana akiangalia saa, akionekana kutokuwa mvumilivu

Bila Uvumilivu: Mafundisho na Maagano 100:15

Kwa hiyo, mioyo yenu na ifarijike; kwani mambo yote yatafanya kazi kwa pamoja kwa manufaa yao wale watembeao wima.

Chapisha