2022
Mahekalu: Lulu ya Thamani Kuu
Julai/Agosti 2022


“Mahekalu: Lulu ya Thamani Kuu,” Liahona, July/Aug. 2022.

Karibu kwenye Toleo Hili

Mahekalu: Lulu ya Thamani Kuu

Picha
Hekalu la Brigham City Utah

Picha ya Hekalu la Brigham City Utah

Ni baraka kuu iliyoje kuona mahekalu yakijengwa kwa kasi kubwa ulimwenguni kote. Tunafurahi pamoja na waumini wa Kanisa pale mahekalu mapya yanapowekwa wakfu katika maeneo yao.

Tunatumaini watu wote watathamini hekalu na kutokuwa mateka wa kosa lililoelezewa na Rais Boyd K. Packer (1924–2015), Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Katika mfano wake wa lulu na boksi, alisimulia kwamba fundistadi alitengeneza boksi zuri la kuonyeshea lulu ya thamani kuu. Watu walipokuja kuona lulu, hata hivyo, walilitamani boksi badala ya lulu. (Ona “The Cloven Tongues of Fire,” Liahona, Julai 2000, 7.)

Ni kweli, lulu ya thamani kuu ndani ya hekalu hujumuisha ibada, maagano na baraka zilizoahidiwa ambazo tunaweza kuzipokea hekaluni pekee. Kama Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anavyofundisha katika toleo hili: “Kila kitu tunachofunzwa na kufanywa katika mahekalu ya siku za mwisho huweka mkazo kwenye mpango mkuu wa furaha wa Baba wa Mbinguni, uungu wa Yesu Kristo na jukumu Lake kama Mwokozi wetu. Maagano yanayopokelewa na ibada zinazofanywa katika mahekalu ni muhimu katika kutakasa mioyo yetu na hatima ya kuinuliwa kwa wana na mabinti za Mungu” (ukurasa wa 6).

Unaposoma makala ya Mzee Bednar, tunakualika ukumbuke maagano uliyofanya hekaluni. Kama muda kidogo umepita tangu ulipohudhuria hekaluni, tunakualika urejee na uhisi shangwe na amani tena inayopatikana katika nyumba ya Bwana. Kama hujawahi kufika hekaluni, tunakualika kujiandaa ili “mjaliwe uwezo kutoka juu” (Mafundisho na Maagano 38:32).

Mzee Kevin R. Duncan

Wa Sabini

Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Hekalu

Chapisha