2022
Kamwe Hauko Peke Yako
Julai/Agosti 2022


“Kamwe Hauko Peke Yako,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.

Njoo, Unifuate

2 Wafalme 6

Kamwe Hauko Peke Yako

Je, umewahi kuhisi mpweke au mwoga kwa lile lililopaswa kutokea? Mtumishi wa Elisha nabii alihisi hivyo pia alipoona jeshi la Shamu la farasi na magari kuzunguka Dothani, mji wa nyumbani wa Elisha.

Picha
Wanajeshi wakielekeza mishale kwenye ukuta

Vielelezo na Denis Freitas

Kwa woga mtumishi alimlilia Elisha, “Bwana wangu, tufanyeje?” (2 Wafalme 6:15).

Picha
Magari ya moto

Kwa imani, Elisha akamjibu, “Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”(Mstari wa 16). Baada ya Elisha kumwomba Bwana kufungua macho ya mtumishi wake, mtumishi aliona “farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.” (mstari wa 17).

“Kunaweza kuwa na nyakati ambapo, kama mtumishi, utajikuta unapata ugumu kutambua jinsi Bwana anavyofanya kazi katika maisha yako—nyakati ambapo wewe utahisi umezingirwa—wakati ambapo mateso ya maisha yatakufanya udhoofike. Subiri na uamini katika Mungu na katika muda Wake, kwa sababu unaweza kuamini moyo Wake kwa moyo wako wote. … Nyie pia mnaweza kuomba ili Bwana afungue macho yenu kuona mambo ambayo kwa kawaida msingeyaona” (Michelle D. Craig, “Macho ya Kuona,” Liahona, Nov. 2020, 15).

Sisi tunaweza tusiyaone, lakini Bwana na jeshi Lake la malaika limetuzunguka (ona Mafundisho na Maagano 84:88). “Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” (Warumi 8:31).

Chapisha