2022
Kuwa na Ujasiri wa Kuwafikia Wengine
Julai/Agosti 2022


“Kuwa na Ujasiri wa Kuwafikia Wengine,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.

Kanuni za Kuhudumu

Kuwa na Ujasiri wa Kuwafikia Wengine

Mungu atatutumia kuleta tofauti kama tutashinda hofu zetu.

watu wawili wakizungumza na kutabasamu

Kama watu wanaoamini, tuna jukumu kubwa la kuwa na ujasiri katika nyakati hizi, hata katika uzoefu wetu wa kuhudumu. John (majina yamebadilishwa) alipangiwa kuhudumu kwa Peter, muumini ambaye hajawahi kuhudhuria vikao vya kata. John alikuwa na hofu kuhusu kuzungumza na Peter, kwani alikuwa hajawahi kumuona na hakujua lolote kumhusu. Lakini kumbuka ushauri wa “kupenda, kushiriki na kualika,” John aliomba mwongozo na kisha kuamua kuwa rafiki wa dhati na Peter. Alitumia muda mwingi kumjua Peter, kwa kumtembelea mara kwa mara, , kumpigia simu na matembezi ya chakula cha asubuhi. John alizidi kumjua Peter vyema na Peter alimuamini katika urafiki wao. Peter alipohitaji msaada, ilikuwa kawaida kwa kumtafuta John, ambaye kwa furaha hakusita kufika.

Siku moja, John alihisi kwamba labda Peter atakuwa tayari kwa mwaliko wa kuja kanisani. Wakati mmoja wa matembezi yao John alitoa wazo katika hali ya kawaida. Peter alisita. “Sijawahi kuwa kanisani kwa miaka 17,” alisema. “Lakini unajua, nadhani nitakuwepo.” Wakati Peter alipofika kwenye kata, John alikuwepo kumkaribisha na kukaa pamoja naye. John alihisi mwenye furaha kwamba aliweza kuachana na woga wake wa mwanzo. Kwa kupitia jitihada hizi, wote wawili walikuwa na urafiki wa dhati uliobariki maisha yao.

Pata Nguvu Mpya

Esta mbele ya mfalme

Esta mbele ya Mfalme, na Minerva Teichert

Hadithi ya Agano la Kale ya Esta (ona Esta 1–10) hufundisha kanuni nyingi lakini huenda hujulikana vyema kama hadithi ya ujasiri. Esta alikuwa ni msichana wa Kiyahudi wakati alipochaguliwa kama malkia na kuonyesha ujasiri mkuu wakati alipohatarisha maisha yake kuwaokoa watu wake.

Kwa njia ya udanganyifu, mfalme alikuwa amedanganywa na kutoa amri kwamba Wayahudi wote wa ufalme huo wataangamizwa. Esta alifikiria mpango ambao ulihitaji imani kuu na inaweza kuwa njia pekee ya kubadili akili ya mfalme.

Katika utamaduni wa mila yake, kwenda kwa mfalme bila kualikwa kungeweza kupelekea adhabu ya kifo. Lakini kwa ujasiri aliendelea na mpango wake na kuwaomba watu wake kufunga pamoja naye (ona Esta 4:16). Kwa kupitia matendo yake ya ujasiri na matendo ya wengine, alifanikiwa kumshawishi mfalme kubadili amri yake. Maombi ya Esta na watu wake yalijibiwa.

Tunaweza kumuangalia Esta kama mfano wa ujasiri, hata katika kuhudumu, tunapoweka pembeni hofu zetu ili kumjua mtu fulani na kuwasaidia kwenye changamoto zao.

Kanuni za Kuzingatia

Ni nini tunaweza kufanya kama tutajikuta nje ya faraja yetu pale tunapohudumu?

Je, Tunaweza Kufanya Nini?

Kuwa na ujasiri wa kuwafikia wengine Iwe labda ni kutaka kumjua mtu fulani au kuwaalika kufanya kitu fulani ambacho kinaweza kubariki maisha yao, Mungu atakusaidia.