“Kweli 5 kuhusu Esta,” Liahona, July/Aug. 2022.
Njoo, Unifuate
Esta
Kweli 5 kuhusu Esta
1. Esta alikuwa ni yatima.
Esta alikuwa Myahudi, na wazazi wake walipofariki, alilelewa na binamu yake, Modekai, ambaye pia alikuwa Myahudi (ona Esta 2:7).
2. Esta aliishi Uajemi.
Esta aliishi Shushani, Uajemi (ambayo ni Iran ya leo), zaidi ya miaka 100 baada ya Wayahudi kuchukuliwa mateka kwenda Babeli.
3. Esta alilazimika kuficha utambulisho wake wa Uyahudi.
Kwa ombi la Modekai, Esta hakuweka wazi urithi wake wa Kiyahudi kwa mtu yeyote. Aliuficha utambulisho wake, hata baada ya kuwa malkia. (Ona Esta 2:10, 20.)
4. Esta alihatarisha maisha yake ili kuwaokoa watu wake.
Wakati wa nyakati za Esta, wafalme mara kwa mara walikuwa katika hatari ya kuuwawa. Kwa hivyo, kwa ajili ya usalama wa mfalme, mila ziliweka kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kwenda kwa mfalme bila mwaliko wake. Ndio maana Esta alihatarisha maisha yake alipomwendea mfalme kumualika kwenye karamu ambayo angeweka wazi mipango ya Hamani ya kuwauwa Wayahudi (ona Esta 5; 7).
5. Esta alikuwa na imani katika Mungu.
Esta aliomba kwamba Wayahudi wote wa Shushani wafunge kwa siku tatu kabla hajaingia kwa mfalme (ona Esta 4:16). Kwa sababu ya ujasiri wa Esta, na baraka za Bwana, Wayahudi hawakuuawa.