“Maandiko Hugeuza Mioyo Yetu kwa Mungu,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.
Njoo, Unifuate
Maandiko Hugeuza Mioyo Yetu kwa Mungu
Rais Spencer W. Kimball alisema kwamba hadithi ya Yosia, inayopatikana katika 2 Wafalme 21–23, “ni mojawapo ya hadithi nzuri sana katika maandiko yote” (katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022, 129).
Jinsi Mfalme Yosia Alivyopata Maandiko
Yosia alikuwa Mfalme wa Yuda alipokuwa na miaka minane tu. Alirithi ufalme wa watu ambao waliamini kwenye miungu ya uongo, lakini alitaka kumfuata Bwana. Katika mwaka wa nane wa utawala wake, aliagiza kwamba madhabahu na sanamu za miungu ya uongo itokomezwe katika Uyahudi yote.
Miaka kumi baadaye, aliwataka watu wake kurejesha hekalu huko Yerusalemu, ambako kuhani mkuu Hilkia alipata maandiko. Mfalme Yosia alipokisoma kitabu, alivuviwa kufuata mafundisho ya kitabu hicho. Kisha alikusanya watu wake na kuwasomea kitabu hicho.
Kwa muda mrefu, watu walikuwa wameshupaza mioyo yao dhidi ya Mungu. Lakini maandiko yalisaidia kugeuza mioyo ya watu kumrudia Mungu. Mfalme Yosia aliwaahidi watu kwamba atatembea katika njia za Bwana na kutii amri.