2022
Nimekuwa Nikikubeba
Julai/Agosti 2022


“Nimekuwa Nikikubeba,” Liahona, Julai/Agosti 2022.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Nimekuwa Nikikubeba

Hisia za dhati zilizonijia zilikuwa zenye nguvu kiasi kwamba zilinifanya nipige magoti.

Picha
msichana mdogo akiwa amefumba macho

Nilikuwa na miaka mitatu tu na sikutaka kuondoka hospitalini, ambapo wazazi wangu walikuwa wakipata matibabu baada ya ajali ya gari.

Picha kwa hisani ya mwandishi; kona za picha kutoka Getty Images

Nimehangaika kwa miaka mingi kwa kiwewe na hofu inayohusiana na ajali ya gari ambayo mimi pamoja na wazazi wangu tuliipata nilipokuwa na miaka mitatu. Kaka yangu ambaye alikuwa hajazaliwa hakunusurika.

Kwenye ukumbusho wa miaka 25 ya ajali, nilipata kurejelea ajali hiyo. Miezi kadhaa baadaye, bado nilihangaika ndipo rafiki alipopendekeza kwamba nimgeukie Baba yangu wa Mbinguni. Nilicheka na kisha nikauliza, “Atafanya nini kwa ajili yangu?”

Mahangaiko yangu yaliendelea. Baada ya mwaka mwingine mmoja au miwili, nilichoka kuumia na maumivu yangu yalikuwa yakigeuka kuwa hasira. Nilichukua ushauri wa rafiki yangu na kuanza kumgeukia Mungu.

“Kama kweli upo, tuma mtu—yeyote yule,” niliomba. “Nahitaji mtu!”

Siku ilianza na kuisha nikiwa nimesimama mlangoni, nikisubiri bila mafanikio.

“Unaona, Mungu, hakuna anayejali!” Nilisema. “Hakuna mtu aliyekuja!”

Machozi yalipokuwa yakinitiririka, taratibu niliingia ndani ya nyumba na kufunga mlango. Nilitembea kupanda ngazi nikihisi kushindwa. Lakini nilipofika mwisho wa ngazi, hisia kali ilinijia. Ilikuwa kali kiasi kwamba ilinifanya nipige magoti.

Kisha wazo hili lilinijia akilini: “ReNae, Nimekuwa nikikubeba.”

Baba wa Mbinguni alituma fikra hiyo nzito kwangu katika njia ya upendo wakati nilipokuwa naihitaji sana. Nilitambua kwamba Yeye kweli ananipenda na Yeye kweli ananijua. Ananipenda sana kwamba amenipa haki ya kujiamulia. Hatanishurutisha mimi wala mwingine yeyote kumfuata Yeye, lakini Yeye na Mwanawe wanatualika kuwafuata Wao (ona Mathayo 11:28–30).

Tangu siku hiyo, najua kwamba naweza kumtegemea Yeye. Maisha yangu yako vizuri sasa kwa sababu najitahidi kumfuata Yeye na kumsikiliza Yeye kila siku. Wakati Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wananiruhusu nihisi maumivu, Wao wananipatia pia amani, faraja, nguvu na ujasiri ili kwamba nijifunze kwa kufanya mambo magumu. Kuhisi maumivu kunanifanya niwaelewe na kuwasaidia wengine walio na changamoto.

Kamwe hatuwezi kujua kwa ukamilifu kile wengine wanachopitia, lakini tunaweza kuonyesha upendo kwa wale wanaotuzunguka. Nina shukrani kwamba ninajua kuwa Baba yangu wa Mbinguni ananipenda na kunisikiliza pale ninapomlilia Yeye.

Chapisha