2022
Bwana Alitunza Ahadi Yake
Julai/Agosti 2022


“Bwana Alitunza Ahadi Yake,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Bwana Alitunza Ahadi Yake

Kwa ajili yangu na familia yangu, baraka za Bwana zilikuja kutokana na utiifu wangu.

Picha
matone ya mafuta yakidondoka kwanye bakuli

Miezi miwili baada ya kuitwa kama mshauri katika urais wa kigingi chetu, nilipoteza kazi yangu. Nilipatwa na wasiwasi kuhusu jinsi ambavyo ningeweza kumkimu mke wangu na watoto wetu wawili.

Wakati nikitafuta kazi mpya, nilijikita kwenye wito wangu, ambao ulinipa fursa nyingi za kuwatumikia kaka na dada zangu. Kwa kweli, nilighubikwa na wito wangu kiasi kwamba mke wangu aliuliza kama kuna yeyote mwingine kwenye kigingi ambaye angeweza kufanya baadhi ya majukumu yangu.

Usiku mmoja wa mvua kabla tu ya jioni ya familia nyumbani, simu iliita. Kaka kutoka kwenye kigingi aliyekuwa mgonjwa sana alihitaji baraka na niliombwa kwenda kumuona. Mara moja, nilifanya mipango ya kupata rafiki wa kuandamana nami.

Tulipofika, mara moja nilimtambua kaka huyo mgonjwa na nilishukuru kwa kupigiwa simu. Siku kadhaa hapo kabla, alikuwa amehojiwa kwa ajili a wito wa kigingi. Baada ya kumpaka mafuta na kumbariki, tulimwambia kwamba tungerejea baadae kumuona.

Niliwasili nyumbani muda ukiwa umeenda na nikiwa nimelowa, lakini bado tulikuwa na muda mchache wa somo la jioni ya familia. Tuliamua kuangalia video kuhusu Eliya na mjane wa Sarepta.

Wakati mjane alikuwa akijiandaa kupika chakula kichache cha mwisho kwa ajili yake na mwanae, Eliya alimwambia, “Unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.” Kwa utii wake, “pipa la unga [halikupunguka], wala ile chupa ya mafuta [haikuisha], hata siku ile Bwana [alipoleta] mvua juu ya nchi.” (1 Wafalme 17:13–14).

Maneno ya Eliya “Unifanyie kwanza” yalipenya moyo wangu. Nikiwa natokwa machozi, nilimwambia mke wangu, “Ndiyo hiyo! Kwanza, lazima tufanye yote ambayo Bwana anaamuru, na kisha baraka zitakuja.”

Kama ilivyokuwa utimilifu wa ahadi ya Eliya kwa mjane, chakula chetu na mafuta “havikuisha” wakati nikiwa sina kazi. Bwana alijua hali yetu ngumu ya kipesa na Alitubariki. Asubuhi iliyofuata baada ya jioni yetu ya familia nyumbani, nilipewa kazi.

Ninajua kwamba Bwana anatunza ahadi Zake. Kwa sababu ya uzoefu huu, imani yangu ni kubwa, kama shukrani yangu Kwake.

Chapisha