2022
Aina za Ufunuo Binafsi
Julai/Agosti 2022


“Aina za Ufunuo Binafsi,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.

Njoo, Unifuate

1 Wafalme 17–19

Aina za Ufunuo Binafsi

Elisha alisimama mlimani na kuona upepo ukivunja miamba na alihisi tetemeko, “na baada ya tetemeko la nchi moto; bali Bwana hakuwemo katika moto: na baada ya moto sauti ndogo tulivu.”(1 Wafalme 19:12). Hizi ni baadhi ya njia tatu ambazo sauti tulivu, ndogo hutuletea ufunuo.

Picha
mkono ukiwasha taa

Wakati mwingine ufunuo binafsi huleta uelewa mara moja, kama vile kuwasha taa katika chumba cha giza.

Picha
mtu akitembea kuvuka ukungu

Wakati mwingine tuna nuru ya kutosha tu kutuchukua hatua chache mbele.

Picha
mtu akitazama kuchwa kwa jua

Wakati mwingine ufunuo binafsi huja pole pole, kama kuchwa kwa jua.1

Chapisha