“Nafasi ya Kukua,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.
Zeeka kwa Uaminifu
Nafasi ya Kukua
Bwana alijua ningechanua na kumea mara nyingine tena.
Imekuwa miaka kadhaa tangu mume wangu, Jerold, alipofariki. Saratani ilikuja kwa kasi na kwa ukali na ndani ya miezi mitatu alifariki. Sasa nilikuwa namfikiria yeye nilipokuwa nashughulika kwenye uwa wangu.
Nilipokuwa nahamisha mmea, nilikuwa na wazo. Kabla ya kuingilia, mmea ulionekana kuwa SAWA. Mmea ulikuwa nyumbani katika chungu, lakini ulikuwa hauchanui. Nilijua kama nisingeuhamisha kwa wakati, huenda ungeacha kuchanua na huenda ungekoma kukua. Mmea usingeweza kukua vizuri.
Hivyo, niliamua kuupatia mmea nafasi ya kukua kwa kuuhamishia kwenye chungu kikubwa. Sio chungu kikubwa sana—ila kikubwa kuzidi cha awali kwa nchi mbili kwa upenyo. Kama ningeupatia nafasi kubwa sana, ungeishia kunywa maji kupita kiasi na kufa kutokana na mizizi kuoza.
Nilitegemea mmea kupitia ugumu unapojaribu kuzoea mazingira mapya. Mmea ulikuwa hauna shida, ulizoea kila kitu kwenye chungu. Mmea haukuwa na taarifa kwamba mabadiliko yangeusaidia kukua. Nilihitaji kuulea, kuupatia mwanga wa kutosha, maji na virutubisho vya ziada vinavyohitajika wakati huu wa mabadiliko. Nilijua hatimaye ungechanua na kutoa maua tena.
Nilipofikiria maisha yangu kama mjane, nilitambua kwamba nilikuwa kama mmea huo. Nilikuwa vizuri. Nilikuwa naendelea vizuri. Lakini mume wangu alipofariki, nilisikia Roho ikininong’oneza kwamba naingia kipindi kipya cha ukuaji. Nilikuwa bado na mambo ya kujifunza na kufanya katika maisha haya.
Kwa miaka miwili iliyofuata, watu wengine saba kwenye kata yetu walifariki. Nilianza kuwaomba marafiki zangu wajane wapya tukiwa pamoja, kuongea, kutembeleana, kutumikiana—ili kwamba kila mmoja wetu angehisi upweke kidogo. Hakuna yeyote kati yetu ambaye angechagua “kuhamishwa chungu.” Lakini baada ya kuzoea maisha ya duniani bila kuwa na mume wangu, niligundua kwamba ningeweza kutoa msaada kwa wengine ambao walipitia changamoto kama hiyo. Pia niligundua kuna fursa nyingi za kutumia muda na watoto na wajukuu na kuwahakikishia kwamba kwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, katika maisha yajayo familia yetu inaweza kuwa pamoja tena.
Kamwe sikutarajia ukuaji ambao ungetokea kwangu kwa sababu ya kumpoteza mwenza wangu. Lakini Baba wa Mbinguni aliingilia kati na “kunihamisha chungu”, kunipa nafasi ya kukua kwa kuniweka kwenye chungu chenye ukubwa zaidi—changamoto mpya ambayo ilileta fursa ya kukua.
Bado namkumbuka Jerold kila siku. Miaka kadhaa baadaye, bado napata shida ninapojaribu kubadilika kwenye hali ya kutokuwa pamoja naye. Lakini najua Bwana atanistawisha kwenye njia yangu. Kwa muda kupita, na kwa tumaini Kwake, nitachanua na kutoa maua tena.
Mwandishi anaishi Idaho, Marekani.