2022
Ibada za Hekaluni: Kujiandaa Kurejea kwenye Uwepo wa Mungu
Julai/Agosti 2022


“Ibada za Hekaluni: Kujiandaa Kurejea kwenye Uwepo wa Mungu,” Liahona, Julai/Agosti. 2022.

Ibada za Hekaluni: Kujiandaa Kurejea kwenye Uwepo wa Mungu

Ninawaalikeni kwa bidii mjifunze kuhusu na kuthamini umuhimu wa milele wa maagano ya hekaluni, ibada za hekaluni na kuabudu hekaluni kadiri unavyojitahidi kusonga kwa Mwokozi.

Picha
Ufunguzi wa wazi wa Hekalu la Mesa Arizona

Picha ya ufunguzi wa wazi wa Hekalu la Mesa Arizona na Leslie Nilsson

Kazi ya Mungu na utukufu Wake ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39)—ili kutuandaa sisi kuishi “katika hali ya juu na tukufu zaidi”1 ili turejee kwenye uwepo Wake.

Katika rehema yake isiyo na mwisho na ya milele, Bwana, kwa kupitia kwa manabii na mitume wake, mara kwa mara amewaalika wana na mabinti Zake wajiandae kwa ujio Wake na kuwa watu wa Sayuni—tukiwa tayari kuinuliwa kukutana naye (ona Alma 12:24; 34:32; Mafundisho na Maagano 45:45; 65:5; 88:96–97). Na siku zote kitovu cha maandalizi hayo imekuwa ni kujifunza mafundisho ya Yesu Kristo, kuwa na imani Kwake, kutubu na kupokea maagano na ibada takatifu.

Mifano kutoka Agano la Kale kuhusu mialiko ya Mungu kwa watoto Wake kujiandaa kuishi sheria ya juu zaidi na kupokea maagano na ibada za wokovu ni vya kutuongoza sisi leo.

Katika kitabu cha Kutoka, Mungu aliwaimarisha Waisraeli kuwa “tunu” na kujisafisha wao wenyewe katika kujiandaa kukutana Naye (ona Kutoka 19:4–6, 10–11, 17). Yehova aliwapa Waisraeli “mbao za mawe na ile sheria na hiyo amri” (Kutoka 24:12), na wakaagana na Mungu wakisema “Hayo yote aliyoyasema Bwana tutayatenda” (Kutoka 19:8; ona pia 24:3). Bwana aliahidi kama watakuwa watiifu kwenye maagano yao, Yeye atakaa miongoni mwao (ona Kutoka 29:45–46). Hata hivyo, wakati Israeli iliposhuhudia “utukufu wa Bwana” (Kutoka 24:16) juu ya Mlima Sinai, waliogopa, wakasimama mbali na hatimaye waliasi dhidi ya Mungu (ona Kutoka 20:18–21; 32:1–6).

Mfano wa pili kwenye Agano la Kale ni wa Mfalme Sulemani akijenga nyumba kwa Bwana (ona 1 Wafalme 6:11–13). Sanduku la agano pamoja na vyombo vingine vitakatifu viliwekwa “patakatifu pa patakatifu” (1 Wafalme 8:6), na “kwa kuwa nyumba ya Bwana ilikuwa imejaa utukufu wa Bwana.” (1 Wafalme 8:11). Sulemani alitoa sala ya kuweka wakfu na aliomba kwa ajili ya baraka za kimwili na kiroho kuwekwa juu ya Israel iliyotubu na yenye kuomba. Bwana alisikia maombi yao na kuiahidi Israel baraka kuu kama watakuwa watiifu. Hata hivyo, Israel ilimuacha Bwana na kuabudu miungu ya uongo. (Ona 1 Wafalme 9–11.)

Manabii wengine kwenye Agano la Kale walitafuta kwa bidii kuifundisha na kuitakasa Israel ili kwamba “waweze kuuona uso wa Mungu; Lakini waliishupaza mioyo yao na kushindwa kustahimili uwepo wake” (Mafundisho na maagano 84:23–24).

Mara kwa mara watoto wa Israel walikuwa hawaamini, waoga au hawakuwa tayari kubadilika; wakitamani njia nyepesi; na mioyo yao iko kwenye vitu vya ulimwengu; au kwa kujua waliasi dhidi ya Bwana na manabii Wake. Kila mara Israel ilipoasi dhidi ya Mungu na kusahau maagano na ibada zao “hasira yake iliwaka dhidi yao” (Mafundisho na Maagano 84:24), na hawangepokea utimilifu wa utukufu Wake.

Lengo la Kiungu la Kukusanya

Juhudi za Bwana za kukusanya watu Wake na kuwabariki kwa kupitia maagano na ibada za hekaluni pia zinasimuliwa katika Agano Jipya na Kitabu cha Mormoni. Mwokozi alilia, “Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!” (Mathayo 23:37; ona pia 3 Nefi 10:4–6).

Nabii Joseph Smith alifundisha: “Ni nini lengo la kukusanya … watu wa Mungu katika kila kipindi cha ulimwengu? … Lengo kuu lilikuwa kumjengea Bwana nyumba ambayo kwayo angeweza kufunua kwa watu wake ibada za nyumba Yake na utukufu wa ufalme Wake, na kuwafundisha watu njia ya wokovu … ili kwamba waweze … kupokea ufunuo kutoka mbinguni, na kufanywa wakamilifu katika vitu vya ufalme wa Mungu—lakini hawakutaka.”2

Bwana anatamani kukusanya watoto Wake katika kipindi hiki na amefunua “mambo ambayo yalifichwa tangu kabla ya kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, … mambo yote yahusuyo nyumba hii, na ukuhani wake (Mafundisho na Maagano 124:41–42). Anatuhimiza sisi sote kujiandaa kurejea kwenye Uwepo Wake—uliofanywa uwezekane kupitia dhabihu Yake ya Upatanisho: “Tazama, ni mapenzi yangu, kwamba wale wote walilinganao jina langu, na kuniabudu kulingana na injili yangu isiyo na mwisho, yawapasa kukusanyika pamoja, na kusimama mahali patakatifu” (Mafundisho na Maagano 101:22).

Kwa Nini Ibada za Hekaluni ni Muhimu Sana?

Mahekalu ni matakatifu sana kati ya sehemu zote za kuabudia. Kila kitu tunachofunzwa na kufanywa katika mahekalu ya siku za mwisho huweka mkazo kwenye mpango mkuu wa furaha wa Baba wa Mbinguni, uungu wa Yesu Kristo na jukumu Lake kama Mwokozi wetu. Maagano yanayopokelewa na ibada zinazofanywa katika mahekalu ni muhimu katika kutakasa mioyo yetu na hatima ya kuinuliwa kwa wana na mabinti za Mungu.

“Na ukuhani huu mkuu huhudumia injili na hushikilia ufunguo wa siri za ufalme, hata ufunguo wa ufahamu wa Mungu.

“Kwa hiyo, katika ibada hizo, nguvu ya uchamungu hujidhihirisha.

“Na pasipo ibada hizo, na mamlaka ya ukuhani, nguvu za uchamungu haziwezi kujidhihirisha kwa mwanadamu katika mwili” (Mafundisho na Maagano 84:19–21).

Ibada takatifu ambazo zinapokelewa kwa kustahili na kukumbukwa daima hufungua njia za mbinguni ambazo kupitia hizo nguvu za uchamungu zinaweza kumiminika katika maisha yetu. Kwa kupokea ibada za ukuhani na kufanya na kutunza maagano matakatifu, sisi tumetiwa nira pamoja na Mwokozi (ona Mathayo 11:28–30)3 na tunaweza kubarikiwa kwa nguvu zaidi ya tulizonazo ili kushinda majaribu na changamoto za maisha tunapojiandaa kurejea kwenye uwepo wa Mungu.

Baraka za Maagano na Ibada za Hekaluni

Picha
mchoro waa Yesu Kristo

Taarifa kutoka Kristo na Mtoto Mdogo, na Carl Heinrich Bloch

Baraka mbili kati ya baraka muhimu zinazopokelewa kutokana na maagano na ibada za hekaluni kuongezeka kwa shangwe na nguvu.

Mkombozi ndio chanzo pekee na cha mwisho cha shangwe ya kudumu. Shangwe ya kweli huja kwa kuonyesha imani kwa Bwana Yesu Kristo, kupokea kwa kustahili na kwa uaminifu kuheshimu maagano na ibada takatifu na kwa kujaribu kuwa waongofu wa dhati kwa Mwokozi na malengo Yake.

Alma alimfundisha mwanawe kwamba utakatifu mkuu na furaha ya maisha yetu hufanywa iwezekane kama tutaoshwa na kusafishwa kwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Ni kwa kuwa na imani tu kwa Mkombozi wetu, kutubu na kushika maagano ndipo tunaweza kupata furaha ya kudumu tunayotamani kuipata na kuihifadhi.4

Tafadhali chukua ahadi ya shangwe kutoka kwa Rais Russell M. Nelson: “Tunawaalika watoto wa Mungu wote kutoka pande zote mbili za pazia waje kwa Mwokozi wao, wapokee baraka za hekalu takatifu, wawe na furaha ya kudumu na kustahili uzima wa milele.”5

Katika siku zetu kadiri nguvu za giza zinavyozidi “na kutisha amani yetu,”6 nguvu ya ulinzi hupatikana kwa kila mmoja wetu katika na kwa kupitia maagano na ibada za hekaluni (ona Mafundisho na Maagano 38:32; 43:16; 76:39–42; 105:11–12, 33; 138:12–15). Nefi aliona katika ono na “aliona nguvu za Mwanakondoo wa Mungu, kwamba zilishuka … juu ya watu wa agano wa Bwana, … na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu” (1 Nefi 14:14).

Katika sala ya uwekaji wakfu Hekalu la Kirtland, Nabii Joseph Smith alimwomba Baba “kwamba watumishi wako wapate kwenda katika nyumba hii wakiwa wamevikwa uwezo wako” na “kwamba hakuna kundi la uovu litakalo … inuka na kuwashinda watu wako ambao juu yao jina lako litawekwa katika nyumba hii” (Mafundisho na Maagano 109:22, 26).

Picha
Hekalu la Kirtland

Nuru ya Utukufu—Hekalu la Kirtland, na Glen S. Hopkinson, isinakiliwe

Kila mmoja wetu anapaswa kujitahidi kujifunza kuhusu na kuelewa vyema nguvu ya ulinzi ya maagano na ibada zinazopatikana katika nyumba ya Bwana—ili kwamba sisi kama wafuasi tuweze “kusimama katika mahali patakatifu, na … kutohamishwa” (Mafundisho na Maagano 45:32) na “muweze kuhimili siku ya uovu” (Waefeso 6:13).

Mwaliko na Ushuhuda

Ninawaalikeni kwa bidii mjifunze na kuthamini umuhimu wa milele wa maagano, ibada na kuabudu hekaluni unapojitahidi kusonga kwa Mwokozi na kupokea baraka ziliahidiwa kwa kupitia Upatanisho wake. Na kwa shangwe nashuhudia kwamba Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo, wanaishi na hamu Yao kubwa ni kwa sisi kurejea kwenye uwepo wao na kushiri utukufu Wao (see Mafundisho na Maagano 97:16; 101:38).

Chapisha