“Kuna Matumaini,” Liahona, Sept. 2022.
Karibu kwenye Toleo Hili
Kuna Matumaini!
Bila kujali changamoto tunazokabiliana nazo, Yesu Kristo ndiye tumaini letu. Mzee Ronald A. Rasband wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anatoa dhima ya toleo la mwezi huu kwa ukweli ule mzuri katika makala yake mpya, “Matumaini na Faraja katika Kristo” (ukurasa wa 4).
Kwa wazazi wengi, ujumbe huo wa matumaini unahitajika hasa wanapofanya kila wawezalo kuwalea watoto wao katika ulimwengu mgumu. Rais Russell M. Nelson amefundisha: “Adui anaongeza mashambulizi yake juu ya imani na juu yetu sisi na familia zetu kwa kiwango cha ajabu. Ili kushinda kiroho, tunahitaji mikakati kinzani na mipango halisi” (“Hotuba ya Ufunguzi,” Liahona, Nov. 2018, 7). Ili kuunga mkono wazazi katika kazi hii takatifu, Kanisa daima linatafuta kutoa nyenzo ambazo zinaeleweka na ni muhimu.
Katika toleo la mwezi huu, mwandishi mwenzangu pamoja na mimi tunashiriki mpangilio kwa ajili ya wazazi ambao utaleta pamoja kanuni za injili na mikakati yenye kutumika ambayo inaweza kuwasaidia wazazi kujenga uhusiano imara na watoto wao, kutunza imani yao, na kujenga umoja (ona “Mpangilio Imara kwa Ajili ya Malezi”kwenye ukurasa wa 10).
Roho Mtakatifu anaweza kutuongoza kwenye matumaini na msaada tunaouhitaji. Mzee José A. Teixeira wa Sabini anafundisha jinsi tunavyoweza kupokea mwongozo mwingi zaidi kupitia Roho Mtakatifu katika “Chagua Kuwa Makini Kiroho” (ukurasa 40).
Tunatumaini toleo hili litakusaidia wewe na familia yako kupata matumaini, kuhisi upendo zaidi, na kupata shangwe kuu zaidi.
Kwa moyo wa dhati,
Maren Daines, JD
Mbobezi katika Sera ya Familia ya Kimataifa na Programu ya Maendeleo