“Tunaweza Kuwasaidia Wengine Wajisikie Kupendwa na Kujumuishwa,” Liahona, Sept. 2022.
Kanuni za Uhudumiaji
Tunaweza Kuwasaidia Wengine Wajisikie Kupendwa na Kujumuishwa
Mwokozi alipitia kukataliwa na alitufundisha sisi jinsi ya kuwafikia wengine.
Sasha ni msichana mkubwa mseja katika kata ya familia, kitu ambacho sio rahisi daima. Anajisikia mwenye furaha na aliyetosheka lakini mara nyingi yuko tofauti—ni mwenye hasiyeonekana sana—awapo miongoni mwa waumini wengine wa kata. Kama wengi wetu, anatamani kukubalika na kustahili kuwa.
Thomas, mtu mzee katika kata, alipangwa kuwa kaka mhudumiaji wake na alisimama na mke wake siku moja ili kuweza kufahamiana na Sasha. Mazungumzo yalikuwa magumu kidogo kwani maongezi yaligeukia kwenye hali yake ya kuwa mseja. Lakini walipokuwa wakiongea, Sasha aliweza kugundua kwamba Thomas na mke wake walikuwa wakijaribu tu kuelewa hali yake na jinsi ambavyo wangeweza kumsaidia.
Wakati mmoja, Thomasi alisema, “naona uwanja wako ungeweza kuhitaji upendo kidogo. Ningependa kukusaidia hilo.”
Taaluma ya Sasha inamweka na shughuli nyingi sana kiasi kwamba kuushughulikia uwanja siyo kipaumbele cha juu kwake. Zaidi ya hayo, yeye hafurahii hilo. Yeye anajua jinsi ya kufanya kazi ya uwanja, na anajua kuwa angeweza kufanya hivyo. Lakini hilo halibadilishi ukweli kwamba anachukia kuifanya kazi hiyo.
Kulikuwa na wakati ambapo swali lake yawezekana lingeumiza hisia zake. Lakini Thomas alitaja kwamba yeye amekuwa jeshini na anaelewa kitu ambacho mwanamke mara nyingi anakifanya yeye mwenyewe wakati mumewe hayupo karibu. Yeye akatambua kwamba Thomas alikuwa tu akitafuta njia ya kuimarisha urafiki wao. Alikuwa akijaribu kuunganisha uzoefu wa maisha yake na wa Sasha na kupata mahali wanapokutana.
Pande zote za uhusiano wa uhudumiaji huu ulijifunza kupenda na kukubaliana kutoka pale walipokuwa, na urafiki wa karibu, na halisi ulianza.
Na uwanja wa bustani ya Sasha ulipendeza sana.
Mfano Mkamilifu wa Kujumuishwa
Katika Agano la Kale, Isaya alitoa unabii kwamba Yesu Kristo angejua barabara inakuwaje kuwa tofauti. Alipitia kutengwa na kutendewa vibaya. “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko” (Isaya 53:3). Kupitia upendo Wake mkamilifu, Yeye anajua jinsi tunavyojisikia na anajua jinsi ya kutusaidia sisi (ona Alma 7:12). Yeye ni mfano kamili wa jinsi tunavyoweza kuwafikia wengine katika upendo ili tuwajumuishe wengine, bila kujali hali zao au muonekano wao.
Kanuni za Kuzingatia
Unapotafuta njia za kuwasaidia wengine wajisikie kwamba wao ni sehemu ya, zingatia kanuni hizi ambazo Mwokozi alifundisha na kuziishi:
-
Kuwa tayari kuwajua watu nje ya wale ambao tayari unawajua (ona Mathayo 5:43–48).
-
Usiogope kujishirikisha na watu ambao yawezekana wanaishi au wanaamini tofauti kama haimaanishi kutia hatarini mafundisho ya Mwokozi (ona Marko 2:14–17; Luka 7:38–50).
-
Kila mmoja anapaswa kujisikia kama sisi tunawataka kanisani (ona 3 Nefi 18:22–32). Kuwepo mahali wanapoweza kujifunza injili ya Mwokozi na kuhisi upendo Wake unaweza kumbadilisha mtu ye yote.
-
Mwokozi anajua kitu tunachohitaji, kwa sehemu ni kwa sababu Yeye anajua jinsi sisi tunavyojisikia (ona Alma 7:11-12). Tunaweza kuonyesha upendo kwa kutafuta kuelewa mapito ya wengine na kujiweka sisi wenyewe katika viatu vyao.
-
Mwokozi alitenga muda wa kuwepo katika kujibu mahitaji ya wale waliomzunguka. Alisimama ili kuwashughulikia wengine hata wakati ambapo alikuwa na mipango ya kuwa mahali pengine (ona Marko 5:22–43).
Je, Tunaweza Kufanya Nini?
Usiache tofauti zikuzuie wewe kuwajua wale ambao unawahudumia. Bila kujali tofauti zetu, kuna hoja ya pamoja ya kuigundua.