2022
Mzee Ezra Taft Benson Akiwatembelea Watakatifu huko Poland
Septemba 2022


“Mzee Ezra Taft Benson Akiwatembelea Watakatifu huko Poland,” Liahona, Sept. 2022.

Hadithi kutoka Watakatifu, Juzuu ya 3

Mzee Ezra Taft Benson Akiwatembelea Watakatifu huko Poland

Mzee Ezra Taft Benson Akiwa Warsaw, Poland

Akiwa amepangiwa na Urais wa Kwanza, Mzee Benson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alikuwa akisimamia juhudi za misaada ya huko Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia Katika miezi 11 yake huko, alisafiri zaidi ya maili 60,000 (96,000 km). Nyuma yake ni magofu ya Warsaw, Poland.

Picha hii ni kwa hisani ya Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jijini Salt Lake

Jioni ya Jumapili tulivu katika majira ya kiangazi ya mwaka wa 1946, na wenza wake katika safari waliendesha gari kupita katika mitaa yenye ukimya wa kutisha ya Zelwagi, huko Poland. Barabara mbaya na mvua kubwa imewanyeshea vikali wasafiri hawa siku nzima, lakini hali mbaya ya hewa ilikuwa hatimaye imetakata wakati wanaume hawa walipokuwa wanakaribia kufika wanakoenda.

Zełwągi wakati fulani ilikuwa sehemu Ujerumani na imekuwa ikijulikana kama Selbongen. Mipaka ya nchi imebadilika baada ya vita, hata hivyo, sehemu kubwa ya Ulaya kati na mashariki imekuja kuwa chini ya utawala wa Umoja wa Nchi za Kisovieti. Katika mwaka wa 1929, tawi lililokuwa likistawi la Selbongen lilikuwa limejenga jengo lake la kwanza la mikutano ya Watakatifu wa Siku za Mwisho katika Ujerumani. Lakini baada ya miaka sita ya vita, Watakatifu katika vijiji walikuwa wakiishi kwa shida kubwa.1

Na ukweli kwamba Mzee Benson alikuwa huko Poland ilionekana kama muujiza. Kukiwa hakuna laini za simu zinazofanya kazi huko Poland, yeye na washirika wake wamekuwa wakihangaika kuwasiliana na maofisa ambao wangeweza kuwasaidia kupata nyaraka ili waingie katika nchi hiyo. Ni baada tu ya sala nyingi na mawasiliano ya mara kwa mara na serikali ya Poland Mtume aliweza kupata visa muhimu.2

Gari lao aina ya jeep lilipokuwa likilikaribia jengo la mikutano la zamani la Zelwagi, watu wengi mitaani walitawanyika na kujificha. Mzee Benson na washirika wake safarini walisimamisha gari lao mbele ya jengo na kushuka kutoka garini. Walijitambulisha wenyewe kwa mwanamke aliyekuwa jirani na wakamwuliza kama wamelipata jengo la kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Macho ya yule mwanamke yalijawa na machozi ya faraja. “Viongozi wa ukuhani wako hapa!” alilia kwa Kijerumani.

Mara moja watu walitoka nje ya milango iliyokuwa imefungwa, wakilia na kucheka kwa furaha. Watakatifu wa Zełwągi wamekuwa hawana mawasiliano na viongozi wakuu wa Kanisa kwa miaka mitatu, na asubuhi hiyo wengi wao walikuwa wamefunga na kuomba ili watembelewe na mmisionari au kiongozi wa Kanisa. Ndani ya saa chache, takribani Watakatifu mia moja walikusanyika ili kumsikiliza mtume akiongea.

Mzee Benson alipokuwa akiongea na Watakatifu, askari wawili wa Kipoland wenye silaha waliingia kanisani. Kusanyiko lilinyamaza kwa hofu, lakini mtume akawaashiria wale askari kukaa kwenye kiti kilichokuwa mbele ya chumba. Katika mazungumzo yake, alisisitiza umuhimu wa haki ya kujiamulia na uhuru wa kuchagua. Askari wale walisikiliza kwa makini, walibaki kwenye viti vyao hadi wimbo wa kufunga, na waliondoka pasipo kufanya tukio lo lote baya. Baadae, Mzee Benson alikutana na rais wa tawi na akaacha chakula na na fedha kwa ajili a Watakatifu, akawahakikishia msaada zaidi uko njiani unakuja.3

Muda mfupi baadae, Mzee Benson aliuandikia Urais wa Kwanza. Alitiwa moyo ili kuona kwamba misaada ya Kanisa inawafikia Watakatifu huko Ulaya lakini walihofia kuhusu magumu ambayo Watakatifu bado wanakabiliana nayo.

“Pengine manufaa mengi ya programu hii nzuri ya Kanisa ya ustawi wa jamii kwa hawa na kwa Watakatifu wetu wengine katika Ulaya haitaweza kujulikana,” aliandika, “lakini maisha ya watu wengi pasipo shaka yamesalimika, na imani, na ujasiri wa wengi wa waumini wetu walio waaminifu kwa kiasi kikubwa umeimarishwa.”4

watu wamekusanyika nje ya kanisa

Waumini wa Kanisa huko Selbongen, Ujerumani (iliyopewa jina jipya Zełwągi, Poland, baada ya vita), wamekusanyika nje ya jengo lao la kanisa karibia mwaka 1930.

Mihutasari

  1. Ezra Taft Benson, “European Mission Report #19,” Aug. 7, 1946, 1, 3, First Presidency Mission Files, CHL; Benson, Journal, Aug. 1 na 4, 1946; Babbel, Oral History Interview, 6; “Elder Benson Reports First Visit to Poland,” Deseret News, Aug. 17, 1946, Church section, 1, 8, 12; Minert, In Harm’s Way, 310; “Selbongen during World War II,” Global Histories, history.ChurchofJesusChrist.org/global-histories.

  2. Babbel, On Wings of Faith, 131–34; Benson, Journal, July 29 and 30, 1946; Aug. 1 na 4, 1946; ona pia Frederick Babbel, “‘And None Shall Stay Them,’” Instructor, Aug. 1969, 104:268–69. Mada: Poland.

  3. Benson, Journal, Aug. 4, 1946; Ezra Taft Benson, “European Mission Report #19,” Aug. 7, 1946, 1, First Presidency Mission Files, CHL; Ezra Taft Benson to First Presidency, Aug. 7, 1946, 2, Ezra Taft Benson Correspondence Files, CHL; Selbongen Branch, General Minutes, Aug. 4, 1896; “Selbongen during World War II,” Global Histories, history.ChurchofJesusChrist.org/global-histories.

  4. Ezra Taft Benson, “European Mission Report #20,” Aug. 24, 1946, 2, First Presidency Mission Files, CHL; ona pia “Red Cross to Cooperate in Distribution of Supplies,” Deseret News, Sept. 7, 1946, Church section, 1, 9.