2022
Jibu Langu la Kitabu cha Mormoni
Septemba 2022


“Jibu Langu la Kitabu cha Mormoni,” Liahona, Sept. 2022.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Jibu Langu la Kitabu cha Mormoni

Nilijaribu sana “kumuimarisha” Mama Wong, lakini alihitaji tu neno la Mungu lililo rahisi, na lenye nguvu

Picha
mama na binti

Mama Wong na Annie

Picha kwa Hisani ya mwandishi

Baada ya kubatizwa mnamo Juni, 2002, nilishiriki imani yangu pamoja na mama yangu. Ingawa Mama Wong mara kwa mara alihudhuria Kanisa pamoja na mimi, hakutaka kujifunza zaidi.

Mwishowe, miaka 10 baadaye Mama Wong alichagua kubatizwa. Nilifurahia sana. Kwa huzuni, miaka michache baadaye, aliacha kuimarisha ushuhuda wake na kutoa udhuru wa kutohudhuria kanisani.

Nilimsihi aje kanisani, lakini hilo lisababisha ugomvi tu. Hatimaye, niliacha kumsukuma ili nisieumiza uhusiano wetu.

Wakati wa mkutano mkuu wa Oktoba 2019, Rais Russell M. Nelson aliwaalika waumini wa Kanisa “kusanifu mpango [wetu] wenyewe” ili kuimarisha ushuhuda wetu juu ya Urejesho.1 Nilipokuwa nikifikiria kuhusu mwaliko wake, nilihisi kwa nguvu sana kwamba ninapaswa kufanya kitu fulani ili kufanya mambo yawe mazuri zaidi kati ya Mama Wong na mimi.

Kwa maazimio ya Mwaka Mpya, niliazimia mimi mwenyewe kusoma Kitabu cha Mormoni pamoja na Mama Wong. Wakati wo wote aliposema macho yake yanauma, nilisema, “Unaweza kunisikiliza tu.” Aliposema anahitaji kuosha vyombo, nilimfuata jikoni na niliendelea kumsomea kwa sauti.

Ilionekana kwamba Mama Wong alisikiliza kwa karibu sana na akakumbuka kile nilichokisoma. Baada ya muda, alichagua kujisomea mwenyewe. Baadae aliniambia kwamba mtu wa kawaida asingeweza kuandika Kitabu cha Mormoni. Hakuwa na shaka kwamba Kitabu hiki ni neno la Mungu. Kwangu mimi, kumwona akienda kutoka kutokukipenda hadi kutaka kukisoma na kutoa ushuhuda juu ya Kitabu cha Mormoni ni muujiza.

Baada ya Mama Wong kubatizwa, niliogopa kwamba alijiunga na Kanisa kwa sababu yangu mimi tu. Lakini sasa alikuwa na ushuhuda wake mwenyewe. Kwa miaka mingi nilijaribu “kumuimarisha,” lakini yote aliyohitaji ilikuwa ni neno la Mungu lililo rahisi, na lenye nguvu.

Ninashukuru kwa ajili ya nabii aliye hai ambaye daima anatupatia mwongozo kwa wakati muafaka. Kama tutafanyia kazi kile anachotufundisha, baraka kubwa zitafuata. Tukio hili lilinionesha mimi ni kwa kiasi gani Bwana anataka kutubariki sisi. Nilichokifanya mimi ni kumsomea mama yangu sura chache kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni. Kisha Bwana akachukulia hapo!

Muhtasari

  1. Ona Russell M. Nelson, “Maneno ya Kufunga,” Liahona, Nov. 2019, 122.

Chapisha