2022
Je, Mimi ni Kijana Mkubwa Pekee Ninayehangaika Kupata Kusudi Langu?
Septemba 2022


“Je, Mimi ni Kijana Mkubwa Pekee Ninayehangaika Kupata Kusudi Langu?,” Liahona, Sept. 2022.

Vijana Wakubwa

Je, Mimi ni Kijana Mkubwa Pekee Ninayehangaika Kupata Kusudi Langu?

Nilijihisi kama vile nimechafua mpango—mpango wangu kwa ajili yangu mimi mwenyewe, na mpango wa Mungu kwa ajili yangu mimi.

Picha
kijana mkubwa mwanamke akipanda matofali

Katika siku yangu ya 25 ya kuzaliwa, nilikuwa nikikipanga chumba changu cha kulala. Nafasi yangu hiyo haikuwa katika utaratibu, na niliendelea kufikiria kuhusu jinsi gani maisha yangu yasivyokuwa katika utaratibu. Sikuwa pale nilipofikiri ningekuwapo katika umri wa miaka 25. Sikuwa pale nilipopaswa kuwa.

Nilifikiria kuhusu jinsi nilivyojisikia kama kijana wa miaka kumi na wakati nilipopata baraka za kipatriaki. Wakati wo wote nisomapo kuhusu ubaadaye wangu, nilivuta taswira ya mtu ambaye alikuwa amekaribia kukamilika. Lakini nilitambua kwamba mimi bado sijakua kuweza kuwa mtu huyo ninayemfikiria. Na nilijiuliza, kama uchanga wangu ungeweza kuniona mimi sasa, je, angevunjika moyo?

Ghafla nikajikuta ninalia machozi. Nilijiona kwamba nimechafua mpango wa maisha yangu. Sikuwa nimefanya kosa lolote kubwa sana, lakini pia nilijihisi sina kitu cha kuonyesha kwenye maisha yangu. Sikuwa na lengo. Kila mmoja alikuwa tayari ameshajipanga, na hapo mimi niko, nikilia kwenye sakafu ya chumba changu cha kulala, nikijisikia kama maisha yangu yote yameharibika.

Nilijisikia mpweke katika kuchanganyikiwa na kukata tamaa kwangu. Lakini hata katika wakati huo, nilijua nisingeweza kuwa kijana kumbwa pekee anayehangaika kupata njia yao. Nilipoongea na wengine, nimegundua kwamba ni watu wachache sana maisha yao yanaishia sawia na kile walichopanga. Na hiyo inanisaidia mimi kujisikia kidogo siko peke yangu.

Hiyo pia inasaidia kunikumbusha mimi mwenyewe kwamba Baba wa Mbinguni hataki mimi nijisikie kama aliyeshindwa. Yeye ananitaka mimi nisonge mbele kwa uthabiti katika Kristo, nikiwa na mng’aro mkamilifu wa matumaini” (2 Nefi 31:20). Anaamini katika uwezo wangu wa kubadilika na kukua kupitia nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi. Ni Shetani pekee ndiye angetaka mimi nijiambie mwenyewe kuwa nimepoteza nafasi ya kuwa mtu ambaye Baba wa Mbinguni anajua ninaweza kuwa.

Kuelewa Mpango wa Furaha

Wengi wetu tunajisikia hatuna matumaini kuhusu siku za baadae nyakati zingine. Na hii inawezakuwa kwa sababu tunauelewa vibaya mpango wa Mungu wa furaha. Inaweza kuwa tunafikiri maisha yetu ni kama mchezo wa video—wenye mistari iliyopangiliwa ambayo unapaswa kuifuata ili ushinde? Lakini hivyo sio jinsi inavyofanya kazi. Kila siku tunafanya chaguzi, tunabadilika, na kukua. Hakuna kitu kinachosimama au kiliganda kuhusu hili. Chaguzi zetu haziwezi kuwa za kushangaza kwa Baba wa Mbinguni, lakini bado ni chaguzi zetu. Tunaandika hadithi zetu sisi wenyewe, pamoja na Yeye, kama tunavyokwenda.

Na kama “tutamwacha Kristo awe mwandishi na mmalizaji wa hadithi [yetu],”1 tunaweza daima kuangalia kwa kujiamini kuelekea mwisho wenye furaha milele.

Nyakati zingine tunafanya makosa au tunapoteza mwelekeo, na kuwa tayari kukubali sisi wenyewe kutangatanga bila kuwa na malengo milele.

Lakini hii ni injili ya matumaini. Ya vitu vilivyopotea na vikaonekana. Ni injili ya kujifunza. Ya msamaha. Ya kujaribu tena Kama Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyofundisha, “Toba siyo mpango usiotumika sana; bali ndio mpango wenyewe.”2

Upendo wa Baba yetu wa Mbinguni ni mkamilifu, na mpango Wake kwa ajili yetu ni mkamilifu pia. Ni mpango mkamilifu kwa watu wasio wakamilifu, uliosanifiwa kwa uangalifu na uelewa wa mahitaji yetu na uwezekano wa kuwa. Kuna nafasi katika mpango Wake kwa ajili ya kuanguka—makosa yetu ya uaminifu na dhambi za kiburi chetu na kutangatanga kwetu nyikani. Na kuna nafasi katika mpango Wake kwa ajili ya ushindi wetu, ambao tunaupata kila wakati tunapomtazama Yeye na kujaribu tena.

Tafuta Kusudi Lako

Nimetumia muda mwingi sana tokea siku yangu ile ya kuzaliwa nikifikiria kuhusu kusudi langu. Bado hasa sijapata kila kitu. Lakini sijisikii hofu tena. Ninajua kwamba Mungu ananijua na kwamba kama nitamgeukia Yeye, atanisaidia kutengeneza maana katika nafasi niliyopo sasa.

Pengine mtu fulani wakati fulani ataipata tiba ya saratani au kumaliza njaa ya ulimwengu wote au kupata amani ya ulimwengu. Lakini mtu fulani leo atamfariji rafiki mwenye kuhuzunika au atamsaidia mgeni anayahangaika au atasali kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi. Na nadhani haya yote yana maana fulani—hata kila kitu.

Ukweli ni kwamba, wengi wetu hatutafanya makuu, makuu ya yaivunjayo—dunia katika maisha haya. Lakini hii haimaanisha kwamba hatuna kusudi. Kusudi letu la mwisho kama watoto wa Mungu ni kuwa kama Yeye alivyo. Na tunakua katika kusudi hilo tunapofanya vitu vidogo vidogo kila siku ili kumfuata Yesu Kristo.

Nimekuja kuhifadhi kwa upendo mkubwa mafundisho ya injili kwamba “kupitia kwa vitu vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka” (Alma 37:6). Ninapotazama nyuma kwenye maisha yangu, sioni kitu cho chote kikubwa. Lakini ninaona “vitu vidogo na rahisi” vingi ambavyo vimefanya tofauti. Na ninajua kupitia neema ya Mwokozi jitihada za imani yangu nzuri ndogo inaandala njia yangu ya kuwa kama Yeye.

Njia ya mtu ye yote haitaonekana sawa sawa na yako wewe. Lakini kama unajaribu kwa kadiri ya uwezo wako kuchukua hatua kuelekea kwa Kristo, njia yako ni nzuri. Mwenyezi Muumba anakuamini wewe, hivyo simama wima na ujiamini wewe mwenyewe. Mungu ana mambo ya kushangaza ghalani kwa ajili yako, na hata unapojisikia kuwa mdogo na rahisi, Yeye “atakusaidia kuwa kitu kikubwa kuliko ulivyowahi kufikiria inawezekana.”3

Mihtasari

  1. Camille N. Johnson, “Mwalike Mwokozi Aandike Hadithi Yako,” Liahona, Nov. 2021, 82.

  2. Neil L. Andersen, katika Sarah Jane Weaver, “Repentance Is Not a Backup Plan; It Is the Plan, Says Elder Andersen” (news story), July 3, 2018, ChurchofJesusChrist.org.

  3. Dieter F. Uchtdorf, “Unafanya Kazi Vizuri!,” Liahona, Nov. 2015, 23.

Chapisha