2022
Uzuri wa Kuzeeka
Septemba 2022


“Uzuri wa Kuzeeka,” Liahona, Sept. 2022.

Kuzeeka kwa Mwaminifu

Uzuri wa Kuzeeka

Bora niwe na sura ambayo inaonyesha mistari ya vicheko na machozi.

Picha
bibi akumkumbatia mjukuu wake

Ninakumbuka kama mtoto nilipokuwa nikitazama mashavu ya bibi yangu yakiwa na mikunjo. Mistari ikikunja kona za macho yake, na mistari midogo ikipamba mdomo wake wa juu. Nilimwuliza ninawezaje kukwepa kupata hii mikunjo.

“Usitabasamu,” yeye alisema. “Na usilie.”

Nilifuata ushauri wake—kwa siku moja. Kisha nikakata tamaa. Je, inawezekanaje mtu ye yote kuishi pasipo kutabasamu au kulia? Nilifanya uamuzi ni bora niwe na sura inayoonyesha mistari ya vicheko na machozi.

Katika Kitabu cha Mormoni Lehi alimfundisha mwanawe Yakobo kwamba tuko hapa duniani ili tupate shangwe (ona 2 Nefi 2:25). Lakini pia alimfundisha kwamba ili kujua shangwe, ni lazima tupitie huzuni (ona 2 Nefi 2:22–23). Nimekuja kuona ushahidi wa vyote viwili shangwe na huzuni, kama ilivyochorwa katika nyuso za wale ambao wameyaishi maisha. Nyuso zao zimebeba hadithi za maisha yao.

Ninakubaliana na mtu aliyesema, “Watu wazee wazuri ni kazi ya sanaa.”1 Baadhi ya watu wanakuza tabia uzeeni ambazo huwafanya kuwa wa kusifika. Kwa mfano, nimechungulia ndani ya macho ya watu wenye-nywele nyeupe, matroni wa hekaluni mwenye mavazi-meupe na kupigwa na nuru ya kushangaza ambayo inang’ara machoni mwao na kung’aa katika nyuso zao wakitabasamu.

Sasa kwamba mimi mwenyewe ninakuwa mwanamke mzee, najifunza kwamba kuna baadhi ya shangwe ambazo huja na uzee. Kwa mfano, nimekuwa mwenye faraja zaidi katika mwili wangu mwenyewe. Ninayo shukrani kwamba bado unafanya kazi! Yawezekana nikawa natembea pole pole zaidi na kuongea pole pole zaidi kuliko nilivyokuwa. Paja langu laweza kuwa laini kidogo, na mikono yangu ni miepesi kuumia. Lakini ninapenda kufikiria kwamba mguso wangu ni wa upole pia.

Ninajua kwamba bado ninaweza kuendelea mbele na kujifunza, kwamba “kanuni yo yote ya akili tuipatayo katika maisha haya, itafufuka pamoja nasi katika ufufuko” (Mafundisho na Maagano 130:18). Na hivyo, ninatazamia kwenye somo ambalo bado ninaweza kujifunza. Je, ni nini zaidi, ninachoweza kuwasaidia wengine—kama vile wajukuu zangu—ili kujifunza kutokana na hadithi za maisha yangu ambazo ninaweza kushiriki nao.

Picha
mke na muwe wakiwa wamekaa pamoja

Picha imewekwa na wana mitindo

Mume wangu na mimi tunaweza zaidi kukubaliana na kujua kwamba sisi, pia, tunaweza bado kujifunza na kukua pamoja. Ndoa yetu imekuwa nzuri zaidi kwa sababu ya dhoruba ambazo tumezikabili kwa pamoja. Watoto wetu wamekuwa na kutufanya tuone fahari au kutufanya tuhofie, hii inategemeana na siku. Wajukuu wanaleta shangwe halisi na kushangilia.

Na pamoja na uzee unakuja kutambua kwamba maisha ya duniani hayadumu milele. Sasa ndio ule wakati wa kufanya mambo yale niliyokuwa nikitarajia kuyafanya. Kama siyo sasa, basi lini? “Tazama, wakati wa maisha haya ndio wakati wa watu kufanya kazi yao” (Alma 34:32). Kwa matumaini, uzeeni tunatambua kwamba sasa ndio wakati wa kusema maneno yasiyosemwa, kuponya uhusiano, na kutekeleza malengo yaliyosalia.

Ninavyoendelea kuwa mzee, ninafikiria juu ya urithi ninaoweza kuwaachia uzao wangu. Ninatumaini kwamba sehemu ya hili itakuwa kwamba kadiri nilivyopitia shangwe na huzuni, nilipata hekima Na kwa sababu ya hilo, nimepata uzuri katika kuzeeka.

Mwandishi anaishi California, Marekani.

Muhtasari

  1. Imehusishwa na Eleanor Roosevelt; ona A–Z Quotes, azquotes.com.

Chapisha