“Tafadhali Jaribu Tena,” Liahona, Sept. 2022.
Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho
Tafadhali Jaribu Tena
Nilikuwa na shughuli nyingi nikifanya mambo mazuri, lakini uhusiano wangu na Bwana uliumia kwa sababu nilipuuza kitu kimoja muhimu zaidi.
Nilipomaliza misheni yangu Januari 2019, nilikuwa na uhakika ningeendelea kila siku kujifunza maandiko. Mwanzoni, ilikuwa kweli. Baada ya kazi ningekuja nyumbani na kujisomea maandiko kama ulivyo mwendo wa saa. Nilifurahi kuweza bado kuendelea kujisomea maandiko na kujifunza kuhusu Mwokozi.
Hilo lilibadilika mnamo Juni 2019 wakati rafiki yangu mvulana aliporejea kutoka kwenye misheni yake. Tulianza kuwa na miadi moja kwa moja na tukawa wachumba miezi sita tu baadae.
Katika shughuli ya kupanga ndoa, kazi, kwenda chuoni, na kuwa pamoja na mchumba wangu, kujifunza kwangu maandiko punde kukadorora na kuwa mara chache kwa wiki. Kwa sababu nilivurugwa na mambo mazuri, bila kutegemea nilipuuzia uhusiano wangu na Bwana.
Mume wangu na mimi tulioana mnamo Novemba 2019. Kufuatia siku zetu za mapumziko, nilijaribu kuanza pale nilipoachia katika maandiko. Kwa miezi michache, mume wangu na mimi kwa mafanikio tulijifunza maandiko pamoja. Kila asubuhi kwa dakika chache tungelisoma maandiko na kujadiliana masomo ya Njoo, Unifuate kabla hatujatoka nje ya mlango na kwenda kazini au shuleni.
Kisha janga la ulimwengu la UVIKO-19 likagonga. Pasipokuwepo ratiba maalumu ya shule na kazi, tukapoteza ratiba yetu ya kujifunza maandiko asubuhi. Tulijifunza mara moja moja tu, na uhusiano wetu na Bwana ukaumia. Hata baada ya makatazo kuondolewa na tukarudi kanisani, bado tunahangaika kujifunza.
Waumini wa Kanisa mara nyingi wanao muda wakati wanapohangaika kusoma maandiko yao kila siku. Maisha yetu yana shughuli nyingi, na tunakabiliwa na changamoto kila siku. Lakini katu hatujachelewa sana kuanza tena.
“Bwana hatarajii ukamilifu kutoka kwetu sisi kwenye hatua hii ya ukuaji wetu wa milele,” alisema Rais Russell M. Nelson. Lakini, aliongeza, sisi sote tunaweza kufanya vizuri zaidi na kuwa wazuri zaidi.”1
Mume wangu na mimi hivi karibuni tuliazimia upya kusoma maandiko yetu. Bado hatujakamilika katika hili, lakini tunajaribu kila siku tuimarishe shuhuda zetu. Ninashukuru kwa nafasi hizi nyingi Bwana anazotupa sisi ili kutubu, kufanya vyema, na kuwa wazuri zaidi.