2022
Likiongozwa na Manabii Wanaoishi
Septemba 2022


“Likiongozwa na Manabii Wanaoishi,” Liahona, Sept. 2022.

Misingi ya Injili

Likiongozwa na Manabii Wanaoishi

Picha
Viongozi wa Kanisa mbele ya sanamu ya Christus

Manabii ni wanaume walioitwa na Baba wa Mbinguni kuzungumza kwa niaba Yake. Wanashuhudia juu ya Yesu Kristo na kufundisha injili Yake Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini katika manabii wote wa kale na wa sasa.

Mungu huongea kupitia Manabii

Manabii wanapokea ufunuo kutoka kwa Mungu. Manabii wanapopokea mwongozo wa kiungu wa kutufundisha sisi, ni sawa sawa kama Mungu angeongea naisi (ona Mafundisho na Maagano 1:38). Tunaweza kuamini kwamba wao wanatuambia kitu ambacho Mungu angetaka sisi tujue.

Manabii Wanafundisha juu ya Yesu Kristo

Picha
Mormoni akiwa na mabamba ya dhahabu.

Mormoni Akifupisha Mabamba, na Tom Lovell

Manabii wote hushuhudia juu ya Yesu Kristo. Wanatufundisha kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu. Wanatufundisha kuhusu Maisha Yake, mfano, na Upatanisho Wake. Na wanatuonyesha jinsi ya kumfuata Yeye na kutii amri Zake.

Majukumu ya Manabii

Manabii wanafundisha injili ya Yesu Kristo. Wanaelezea baraka tunazopokea tunapotii amri na matokeo tunayopokea tunapokosa kufanya hivyo. Nyakati zingine, wanaweza kuongozwa kutoa unabii kuhusu matukio ya siku zijazo.

Manabii wa Kale

Picha
Musa akiwa na mbao za mawe

Musa na Mbao za Mawe, na Jerry Harston

Mungu amewafundisha watu kupitia manabii tangu mwanzo. Manabii walioishi katika Agano la Kale ni pamoja na Adamu, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Isaya, na wengine. Palikuwepo pia manabii miongoni wale wa Kitabu cha Mormoni. Manabii hawa ni pamoja na Lehi, Mosia, Alma, na Moroni. Tunaweza kujifunza kitu walichofundisha kwa kusoma maandiko.

Manabii wa Kisasa

Joseph Smith alikuwa nabii wa kwanza katika nyakati za sasa. Alirejesha Kanisa la Yesu Kristo duniani. Russell M. Nelson ni nabii na Rais wa Kanisa hili leo. Washauri wake katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili nao pia ni manabii, waonaji na wafunuzi.

Msikilize Nabii

Picha
wanandoa wakitazama mkutano kwenye simu ya mkononi

Nabii anaongea na sisi wakati wa mkutano mkuu na nyakati nyingine. Anatufundisha kitu ambacho Mungu anatutaka tujue na jinsi ya kumfuata Yesu Kristo leo. Tunaweza tukayapata mafundisho yake katika gazeti la Liahona na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Baraka za Kumfuata Nabii

Tutabarikiwa endapo tutafuata mafundisho ya nabii. Tunapomfuata nabii, tunaweza kujua kwamba sisi tunafanya kitu ambacho Mungu angependa tufanye. Tunaweza kuhisi amani katika maisha yetu na kusogea karibu zaidi na Yesu Kristo.

Chapisha