2022
Thibitisha Kwamba Ninyi Mnahusiana
Septemba 2022


“Thibitisha Kwamba Ninyi Mnahusiana,” Liahona, Sept. 2022.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Thibitisha Kwamba Ninyi Mnahusiana

Nilifikiri Bwana alitaka lisilowezekana, lakini mimi nilikuwa nimekosea.

Picha
kioo kuzi na chati ya nasaba

Jirani yangu bibi mkongwe na mwanae waliishi nyumba chache tu chini kutoka kwa familia yangu. Alikuja kuwa kipenzi chetu. Baada ya mwanawe kufariki dunia, akawa mgonjwa na alilazimika kubaki kitandani. Tulimtunza hadi alipofariki dunia miezi mitatu baadae.

Baada ya kufariki kwao dunia, nilitaka ibada za hekaluni zifanyike kwa ajili ya familia hii. Lakini kwa kuwa hatukuwa na uhusiano, hiyo haikuwezekana. Siku moja wazo zuri likanijia akilini, “Thibitisha kwamba ninyi mnahusiana, na wewe unaweza kufanya kazi za hekaluni kwa ajili yao.”1 Nilifikiri Bwana alikuwa anataka lisilowezekana, lakini neno thibitisha liliendelea kuja akili mwangu.

Ndugu wa jirani yetu huyu wakaanza kuhamisha umilki ya ile nyumba yake, lakini wakakosa kumbukumbu za kuthibitisha uhusiano wao na marehemu, hata baada ya kupekua kumbukumbu za serikali.

Roho akaniambia tulikuwa tunakosa kitu fulani. Kwa ridhaa ya ndugu zake hawa, nilitafuta nyaraka katika nyumba ya yule marehemu Kwenye kona ya ile nyumba nilipata masanduku yaliyojaa makaratasi ya zamani. Nilipata hisia kwamba mifuko ile ilikuwa muhimu.

Niliipekua mifuko miwili kisha nikaanza kupekua wa tatu. Nilikuwa nakaribia kufikia chini kabisa ya mfuko nikahisi kugusa jalada la daftari. Ndani ya mfuko wa jalada la daftari, nilikuta vyeti vitano muhimu: cheti cha kuzaliwa cha jirani yangu mwanamke, vyeti vya kifo na cha ndoa vya mama yake, cheti cha kifo cha mama yake, na cheti cha mazishi ya baba yake.

Wakati ndugu wa jirani na mimi tuliporejelea zile hati, maneno mawili yalikuwa wazi sana kwangu: “Vagaysky District,” huko magharibi mwa Siberia. Ghafla, nikahisi kwamba napaswa kuangalia mti wangu mwenyewe wa familia. Nilipofanya hivyo, niliona kwamba Vagaysky ilionekana kwenye matawi ya mbali ya mti wa familia ya baba yangu. Utafiti zaidi ulionyesha kwamba marehemu jirani yangu na mimi tulikuwa na uhusiano!

Bwana hakuhitaji kitu kisichowezekana kutoka kwangu kumbe. Siwezi kuelezea shangwe yangu ya kujua kwamba jirani yangu ni sehemu ya familia yangu. Kiungo hiki kitaniruhusu mimi kuhakikisha ibada zake za hekaluni zinafanyika siku za usoni.

Bwana anawapenda watoto Wake. Aliandaa mpango wa wokovu kwa ajili ya wote, ikijumuisha na jirani yangu na mwanawe.

Muhtasari

  1. Kama marehemu alizaliwa ndani ya miaka 110 iliyopita na mtu anayetaka kufanya ibada siyo ndugu wa karibu, ruhusa lazima itolewe na ndugu wa karibu wa marehemu (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 28.1, ChurchofJesusChrist.org).

Chapisha