2022
Kutafuta Mwongozo wa Kiroho
Septemba 2022


“Kutafuta Mwongozo wa Kiroho,” Liahona, Septemba 2022.

Kwa ajili ya Wazazi

Kutafuta Mwongozo wa Kiroho

Picha
familia ikisali

Wapendwa Wazazi,

Katika toleo hili la gazeti, viongozi wakuu wenye mamlaka watatu wanashiriki mafundisho na uzoefu wao binafsi na wa familia zao juu ya jinsi ya kutafuta, kupata, na kufuata mwongozo wa kiroho.

Majadiliano ya Injili

Kutegemea Shuhuda Zetu

Kwenye ukurasa wa 4, Mzee Ronald A. Rasband anasimulia hadithi kutoka kwenye historia ya familia yake ili kufundisha kanuni kwamba Mwokozi wetu hatatuacha. Someni makala yake na jadilianeni jinsi Watakatifu wa mwanzo walivyotegemea shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni.

Kushauriana na Bwana

Kwenye ukurasa wa 30, Mzee Patricio M. Giuffra anaelezea jinsi yeye, kama kijana mwongofu kwa Kanisa, alivyoamua kutumikia misheni na kutafuta elimu ya chuo. Kisha anaelezea jibu lake kwa swali, Je, unafanya nini wakati ufunuo binafsi unapoingia kwenye mgogoro na akili ya kawaida?

Kupokea Mwongozo kutoka kwa Roho

Je, tunawezaje kwa ukamilifu zaidi kunufaika kutokana na kipawa cha Roho Mtakatifu katika maisha yetu? Mzee José A. Teixeira anainyambua mada hii kwenye ukurasa wa 40. Soma makala yake na jadilianeni jinsi ya kupokea kwa wingi zaidi mwongozo wa Roho.

Njoo, Unifuate Burudani ya Familia

Itafakari Njia

Mithali 3–4

  1. Weka picha ya Mwokozi juu upande mmoja wa eneo lililo wazi au chumba.

  2. Simama upande ulio mkabala na picha humo chumbani. Fanyeni kwa zamu ya kuziba macho ya kila mwanafamilia, muwazungushe kwenye mduara, na kisha kuona kama wanaweza kutembea kwenda iliko picha ya Yesu Kristo pasipo kupata msaada wo wote.

  3. Soma Mithali 4:26–27.

Jadilianeni: Je, ni aina gani za msaada tumewahi kupewa katika maisha haya ili kutuweka kwenye njia ambayo hutuongoza kwa Yesu Kristo? Kwa majadiliano zaidi, someni Mithali 3:5–6. Je, ni matendo gani tunahitaji kutenda ili kumtumaini Bwana kwa mioyo yetu yote?

Chapisha