2021
Kinanda cha Prophet
Machi 2021


Kinanda cha Prophet

Hadithi hii ilitokea huko Greater Accra, Ghana.

Kijana aliyeitwa Prophet alikuwa na malengo mawili muhimu.

“Muziki ni lugha inayoeleweka na kila mtu” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, iii).

Picha
hands on piano keyboard

Prophet alipenda muziki. Hasa alipenda nyimbo za Msingi na nyimbo za Kanisa. Aliziimba tuni zake siku nzima. Alijiona amekaa kwenye kinanda, huku akipiga nyimbo anazopenda. Pia alijiona akiwafundisha wengine kupiga kinanda.

Kulikuwa na tatizo moja tu. Hakuwa na kinanda.

Siku moja Propeht alikuwa na mahojiano na askofu wake.

“Je, umeweka malengo yoyote kuhusiana na mpango wa Watoto na Vijana?” askofu aliuliza.

“Ndio,” Prophet alisema. “Ningependa kujifunza kupiga kinanda.”

“Hilo ni lengo nzuri,” askofu alisema.

“Na nitakapotimiza lengo hilo,” Prophet alisema, “nitaweka lengo lingine. Ningependa kuwafundisha watu wengine 20 kupiga kinanda.”

“Una malengo mawili mazuri,” askofu alisema.

“Na ninalo tatizo,” Prophet alisema. “Sina kinanda.”

“Wacha tuone kile tunachoweza kufanya.”

Jumapili iliyofuata wakiwa kanisani, askofu alimwambia Prophet kuwa amewapata wamisionari wanandoa ambao wangeweza kumfundisha. Wao wataleta vinanda ili yeye na wengine wajifunze. Wangependa kuwafundisha watu wengi kupiga kinanda.

Askofu alizungumza na watu. Prophet alizungumza na watu. Familia ya Prophet ilizungumza na watu. Baada ya muda, kata yote ilikuwa inazungumza kuhusu watu madarasa ya kupiga kinanda. Hivyo na wengine nao walizungumza.

“Wengi wa marafiki zangu ambao si waumini wanataka kujifunza pia,” Prophet alimwambia askofu.

“Wanakaribishwa, ndiyo” askofu alisema. “Wamisionari watakupa kitabu na watakusaidia kujifunza masomo yake. Na baada ya kujifunza, unaweza kuwasaidia wao kumfundisha mtu mwingine ye yote.”

“Hilo ndilo lengo langu la pili!” Prophet alisema.

Baada ya muda, Prophet alikuwa anafanya mazoezi na wamisionari. Alipenda kujifunza kile ambacho kila noti ilimaanisha nini na kuzisikiliza zikija pamoja ili kufanya wimbo. Marafiki wake wengine wawili ambao ni waumini, Kelvin na Alexander, pia walikuwa wakijifunza. Baada ya mwezi mmoja, wavulana hawa wote watatu walianza kufundisha pia.

Kila siku, wavulana hawa walifundisha madarasa ya kupiga kinanda kwenye jengo la Kanisa. Mwanzoni kulikuwa na karibia wanafunzi 10, halafu 20, halafu 50!

“Hii inafurahisha!” Kelvin alisema siku moja wakati darasa lilipokwisha.

“Nadhani Baba wa Mbinguni amefurahi kwa sababu tunawasaidia wengine kujifunza,” Alexander alisema.

Prophet alitikisa kichwa. Lengo lake tayari lilikuwa linawasaidia watu wengi.

Lakini kuna jambo lingine lililomfurahisha Prophet. Wanafunzi wengine walipokuwa wakifanya mazoezi nyimbo za Msingi, walikuwa pia wanajifunza kuhusu Baba wa Mbinguni. Baadhi yao walimwuliza Prophet kama wangeweza kujifunza zaidi kuhusu Kanisa.

Na ukweli ni kwamba, baadhi ya watu ambao kwanza walijifunza kuhusu Kanisa kwa sababu ya masomo ya kinanda waliishia kubatizwa.

“Sasa katika mikutano,” Nabii anasema, “sote tunaungana pamoja na kuimba nyimbo tunazopenda.”

Chapisha