2021
Ahadi ya Ubatizo Wangu
Machi 2021


Ahadi ya Ubatizo Wangu

Kwa upendo [robo noti] = 108

Picha
sheet music

1. Yesu alimpenda Baba Yake wa Mbinguni

Na alimtii kikamilifu,

Aliungana na Yohana katika maji ya Yordani,

Alibatizwa kwa mamlaka.

Alionyesha njia; Nitamfuata

Kutoka majini hadi nyumbani kwangu mbinguni tena.

2. Ninapobatizwa kwa kuzamishwa majini,

Ninaahidi kuwa kama Yeye,

Kuwapenda na kuwafariji wale wenye shida na

Kusimama kwa ajili ya Kristo po pote nilipo.

Roho Mtakatifu ataongoza njia yangu

Ninapojaribu kumheshimu Mwokozi wangu kila siku.

3. Baada ya kuwa nimefanya ahadi hii,

nitaendelea kwa uaminifu

Kwenye njia ya kushika agano,

Nikitafuta nuru na amani kuu.zaidi

Nikitubu na kumkumbuka Yeye

Kupitia sakramenti, ninaweza kuhisi nimeoshwa safi tena.

Chapisha