2021
Yesu Alihubiri Injili
Machi 2021


Kusaidia Kama Alivyofanya Yesu

Yesu Alihubiri Injili

Picha
Jesus with disciple holding basket of bread

Watu wana njaa wakati miili yao inapohitaji chakula. Huwa na njaa tofauti wanapokuwa na haja ya kusikia injili.

Siku moja maelfu ya watu walimjia Yesu. Yesu aliwalisha wote kwa mikate mitano na samaki wawili.

Siku iliyofuata, watu walimjia Yesu tena. Yesu aliwaambia watafute mkate wa aina tofauti. “Mimi ndiye mkate wa uzima,” alisema. Watu wakimpata Yeye na kupokea injili Yake, roho zao hazitaona njaa kamwe.

Wakati mmoja nilimwambia rafiki yangu, “Mimi huenda kanisani na kujifunza kuhusu Mwokozi wetu Yesu Kristo.” Baadaye alianza kuja nasi kanisani. Alisema kuwa angependa kubatizwa haraka sana! Hilo lilinifurahisha ndani mwangu.

Mary E., miaka 8, Utah, Marekani

Chapisha