2021
Kadi za Historia ya Kanisa
Machi 2021


Kadi za Historia ya Kanisa

Fahamu kuhusu watu muhimu katika historia ya Kanisa! Kata kadi, zikunje kwa kufuata mistari ya nukta kisha zifunge kwa kuzigundisha.

Picha
cut out cards

Mashahidi Watatu

“Tuliona na tunashuhudia kuwa vitu hivi ni vya kweli.”

“Ushuhuda wa Mashahidi Watatu,” Kitabu cha Mormoni

  • Oliver Cowdery, David Whitmer na Martin Harris walikuwa marafiki wa Nabii Joseph Smith.

  • Walimwona malaika, aliyewaonyesha mabamba ya dhahabu. Waliandika ushuhuda wao. Unaweza kuusoma baada ya utangulizi wa Kitabu cha Mormoni.

  • Walikuwa ni baadhi ya watu wa kwanza kubatizwa kuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Lucy Mack Smith

1775–1856

“Kitabu hicho kililetwa kwa nguvu ya Mungu.”

Lucy Mack Smith, Historia ya Joseph Smith (Bookcraft, 1958), p. 204

  • Alikuwa mama yake Joseph Smith.

  • Aliwafundisha watoto wake kuhusu Mungu. Waliomba na kusoma Biblia pamoja.

  • Aliongoza kikundi cha Watakatifu kwenda Kirtland wakitumia mashua. Maji yalipogeuka barafu, aliwahimiza Watakatifu kuomba. Barafu ilipasuka na mashua iliweza kupita!

Vielelezo na Brooke Smart

Chapisha