2021
Kuhisi Upendo wa Kristo
Machi 2021


Rafiki kwa Rafiki

Kuhisi Upendo wa Kristo

Kutoka kwenye Mahojiano na Haley Yancey.

Picha
Friend Magazine, 2021/03-04 Mar/Apr

Nilipokuwa ninakua nchini Japani, nilipewa Biblia shuleni. Ilikuwa na maneno ya Kiingereza na Kijapani sambamba kila upande. Mwalimu wetu mkuu alituambia tuitumie kujifunza Kiingereza.

Nilipokuwa nikiisoma, nilijifunza kuhusu Yesu. Huyu ni mtu gani aliye aliyejaa upendo? Nilijiuliza. Maneno yake aliyoyasema yalinifurahisha. Nilitaka kujua zaidi kuhusu Yeye.

Muda kidogo baadaye, nilikutana na wamisionari. Walinipa Kitabu cha Mormoni na wakanieleza nikisome na niombe juu ya hicho kitabu. Nilipenda kusoma kuhusu Yesu katika Kitabu cha Mormoni. Niliomba na nikahisi kwamba kilikuwa cha kweli.

Hakuna yeyote katika familia yangu aliyetaka kufahamu kuhusu Kanisa. Yesu alifundisha kuwa tunapaswa kuwaheshimu wazazi wetu, lakini wazazi wangu hawakutaka nijiunge na Kanisa. Hilo lilikuwa gumu.

Niliwaambia wazazi wangu jinsi nilivyojisikia. Niliwaambia kuhusu maombi yangu. Hawakuelewa. Walishangaa kwa nini nilitaka kuachana na dini yetu.

Niliendelea kujaribu. Hatimaye wazazi wangu walisema kuwa ninaweza kubatizwa. Miaka mingi baadaye, mama yangu alibatizwa pia.

Ninajua kuwa nilibarikiwa kwa kutamani kumfuata Yesu. Napenda kujifunza kuhusu Yeye na ninajua kuwa kumfuata huleta baraka.

Yesu Anataka Nimfuate Yeye

Picha
coloring page of Jesus being baptized

Yesu anataka tumfuate Yeye kwa tubatizwe. Soma mistari hii. Kisha upake rangi kwenye maumbo yanayooana.

  1. Mafundisho na Maagano 19:23

  2. 2 Nefi 31:12

  3. Mathayo 3:16–17

  4. Mafundisho na Maagano 33:11

  5. Alma 7:15

Chapisha