2021
Hisia Nzuri
Machi 2021


Hisia Nzuri

Mwandishi anaishi Guatemala, Guatemala.

“Nitakuzingira na mikono yangu ya upendo” (Mafundisho na Maagano 6:20).

Picha
A young Guatemalan boy in the font after being baptized hugging his father. Boy in bed with stomach pains Boy in hospital bed with his parents at his side.

Ilikuwa asubuhi angavu na ya kupendeza katika San José Pinula, mji mdogo karibu na Jiji la Guatemala. “Siwezi kusubiri!” Joshua alimwambia dada yake mdogo. Leo ilikuwa siku yake ya ubatizo!

Baada ya familia kuwasili kanisani, Joshua na baba walivalia mavazi meupe. Mwanzoni, Joshua alijisikia woga. Lakini Baba alimshika mkono wake walipokuwa wakitembea kushuka kwenye ngazi za kisima cha maji ya ubatizo, na hakujisikia kuogopa tena kama awali. Wakati Joshua alipokuja kutoka majini, alikuwa na tabasamu kubwa usoni.

Joshua na Baba walibadilisha na kuvaa mavazi makavu. Kisha Baba na wajomba na babu yake Joshua wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha Joshua. Wakamthibitisha kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Joshua alimsikia Baba akisema, “Pokea Roho Mtakatifu.”

“Nina furaha sana!” alisema huku akimkumbatia Baba.

“Kumbuka ahadi ulizoweka leo,” Baba alisema. “Ukizitimiza, Roho Mtakatifu anaweza daima kuwa nawe. Hakika kamwe hutawahi kuwa peke yako.”

Asubuhu moja miezi michache baadaye, Joshua aliamka akilia. Alikuwa na maumivi makali tumboni! “Mama!” Joshua alilia kutoka kitandani. “Tumbo langu linauma sana!”

Tumbo lake liliendelea kuuma zaidi na zaidi. Hakuweza hata kutembea. Baba alimpa Joshua baraka ya ukuhani, kisha yeye na Mama walimpeleka kumwona daktari.

Daktari alisema kuwa Joshua anahitaji kufanyiwa upasuaji mara moja. Ilikuwa inaogopesha.

“Tutakupeleka kwenye chumba maalum ili ufanyiwe upasuaji,” alisema daktari. “Hutajisikia chochote, kwa sababu utakuwa umelala. Wazazi wako watakusubiri hapo nje tu.”

Joshua alihisi woga zaidi. Kwa nini wazazi wake hawakuweza kukaa naye chumbani? Hakuweza kuacha kulia.

Mama alizungumza kwa upole. “Je, tunaweza kufanya nini ili kukusaidia ujisikie vizuri zaidi?” alisema.

“Ninajua tunachoweza kufanya,” yeye alisema. “Tafadhali tuimbe pamoja ‘Mimi ni Mtoto wa Mungu’. Kisha tuombe tena.”

Walipokuwa wakiimba kwa sauti ya chini, Joshua alikumbuka akiimba wimbo huo alipokuwa akibatizwa. Na walipokuwa akiomba, alifikiria kuhusu alichoambiwa na Baba siku ya ubatizo wake: “Roho Mtakatifu anaweza kuwa nawe daima. Hakika kamwe hutawahi kuwa peke yako.”

Joshua bado alihisi woga wakati wauguzi walipompeleka kwenye chumba cha upasuaji. Hakuweza kuona nyuso za madaktari na wauguzi kwa sababu walikuwa wamevalia barakoa. Lakini alipotazama machoni mwao, alifahamu kuwa walikuwa marafiki zake na wangemshughulikia vizuri.

Baada ya upasuaji wake madaktari walisema kuwa Joshua angehitaji kupumzika. Bado alikuwa mchovu na mwenye kuumwa lakini maumivu ya tumbo yalikuwa yamepungua. Hakujisikia kulia tena. Alijua kuwa atakuwa sawa.

“Nilihisi kitu moyoni mwangu,” Joshua aliwambia Mama na Baba. “Ilikuwa hisia nzuri.”

“Hio ni mojawapo ya njia za kumsikia Roho Mtakatifu,” alisema Mama.

Joshua alitikisa kichwa. Nilifurahi kuwa alikuwa na kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa sababu ya Roho Mtakatifu, hakika kamwe hatakuwa peke yake.

Chapisha