Mikono ya Usaidizi kote Ulimwenguni
Kutana na Raiarii kutoka Tahiti
Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.
Yote kuhusu Raiarii
Miaka: 9
Kutoka: Tahiti
Lugha: Kifaransa
Familia: Mama, Baba, kaka watatu na dada mmoja
Malengo na ndoto: 1) Kujifunza kupiga kinanda. 2) Kusoma Kitabu chote cha Mormoni. 3) Kuwa daktari au rubani.
Mikono ya Usaidizi ya Raiarii
Raiarii anapenda kumtembelea bibi yake, Mamy. Anaweza kucheza ufukoni mwa bahari na kuvua samaki kwenye maji mafu. Hula maembe na ndizi kutoka kwenye miti. Miaka michache iliyopita, alikutana na marafiki wa Mamy, Kali na Mia.
Kila asubuhi Raiarii na Mamy wangesoma pamoja Kitabu cha Mormoni. Kali na Mia walianza kujiunga nao. Raiarii alisaidia kufafanua maandiko hivyo ilikuwa rahisi kuelewa.
Raiarii na ndugu zake walipenda kumsaidia Kali kuvua samaki. Siku moja Raiarii alisema, “Hebu tuombe ili tuwe salama na tuvue samaki wengi.” Siku hiyo Kali alivua samaki wengi zaidi kuliko kabla ya hapo! Kali aliamua kuomba daima kabla ya kwenda kuvua.
Raiarii alikuwa anajiandaa kubatizwa. Alimweleza Kali yote kuhusu jambo hilo. Kisha wamisionari walikuja na kuwafundisha Kali na Mia mengi zaidi kuhusu injili. Wakati Kali na Mia wakibatizwa, Raiarii alikuwepo. “Nina furaha sana kuwa Kali alitaka kufuata katika hatua za Yesu,” alisema.
Mambo Ayapendayo Raiarii
Mahali: Nyumbani kwake Mamy
Hadithi kuhusu Yesu: Alipolisha umati kwa samaki wawili na mikate mitano
Wimbo wa msingi: “Ninajua Mwokozi Wangu Ananipenda“ (Rafiki, Machi 2015)
Chakula: Sashimi iliyoandaliwa kwa samaki mbichi aliyevuliwa baharini na keki ya chokoleti iliyotokana na maelezo ya mapishi ya babu na bibi wa baba yake
Rangi: Nyekundu
Somo shuleni: Hisabati