Kujiandaa kwa ajili ya Pasaka
“Mwabudu Baba kwa jina lake, na mikono safi na mioyo mieupe” (2 Nefi 25:16).
“Amka Lydia,” Mama alisema. “Leo ni Alhamisi Safi!” Katika Urusi, mahali ambako Lydia aliishi, Alhamisi Safi ilikuwa ni siku maalum ya kujiandaa kwa ajili ya Pasaka.
Lydia alijigeuza na kutazama dirishani kwake. Nje bado kulikuwa na giza.
“Mama, nimechoka sana,” Lydia alisema. “Je, naweza kulala tena kidogo na nifanye kazi baadaye?”
Mama alitabasabu na akiwa kaketi kitandani. “Kuna sababu ya kuamka mapema leo. “Unajua ni sababu gani?”
Lydia aliwaza sana, lakini hakujua.
“Tunafanya kazi kwa bidii ili kufanya nyumba yetu leo iwe safi ili kujikumbusha jinsi Yesu alivyowaosha wanafunzi wake miguu. Yeye aliwapenda na kuwahudumia watu wengine, na sisi tunataka kuhudumu katika nyumba zetu kama vile Yesu alivyofanya. Leo ni siku ya kumkumbuka Yesu!” Mama alisema.
Lydia alitaka kuhudumu kama vile Yesu, hivyo aliruka kutoka kitandani. Siku hiyo yote, alifanya kazi kwa bidii. Alisafisha sakafu, akafua nguo na akasaidia kupika chakula. Mwisho wa siku aliona fahari. Kila kitu kilikuwa kisafi.
Siku iliyofuata ilikuwa Ijumaa Kuu. Lydia, Mama na Baba walitengeneza mayai ya Pasaka. Walitoboa maganda ya mayai na wakatoa viiniyai vyote. Walichora michoro kwenye mayai kisha wakafunika michoro kwa kutumia nta. Kisha wakayachovya mayai hayo kwenye rangi angavu nyekundu, zambarau na kijani. Lydia alivutiwa na urembo wa michoro yote.
Mayai yalipokauka, Lydia alichukua picha ndogo za familia yake kisha akaziweka ndani ya kila yai. Ijumaa ya leo ilikuwa siku ya kuwa pamoja na kukumbuka dhabihu ya Yesu. Ilikuwa siku ya wiki ambapo Yesu aliiaga dunia. Mayai yalimkumbusha Lydia kuhusu kaburini ambamo mwili wa Yesu ulilazwa. Familia ya Lydia walifanya yote waliyoweza ili kumkumbuka Yeye.
Jumamosi Takatifu, Mama alitengeneza kulich (mkate unaoliwa siku ya Pasaka). Kutengeneza kulich ilikuwa desturi muhimu ya Pasaka nchini Urusi. Watu daima walijaribu kuwa wenye heshima wakati kulich ikiokwa. Lydia aliwaza kuhusu familia yake, Kufufuka kwa Yesu, na mambo ambayo kwayo anayoshukuru. Ilikuwa rahisi kuwazia mambo ya kiroho wakati nyumba yake ikiwa safi na kukiwa na utulivu.
Jumapili ya Pasaka hatimaye ilifika! Lydia alikuwa na furaha sana. Binamu zake walikuja kutembea. Wote walikula chakula kitamu ambacho alikuwa amesaidia kupika. Kulikuwepo na pai, kulich, soseji na jibini. Walipokuwa wakila, walitoa ushuhuda zao na wakazungumzia mambo ambayo kwayo wanashukuru.
Baada ya mlo huo rasmi walicheza mchezo maalum. Kila mtu anashikilia yai lililopambwa na analigonganisha na yai lingine. Mtu ambaye yai lake litapasuka kwanza ndiye ameshindwa. Lydia alitetemeka mikono alipokuwa akigonganisha yai lake dhidi ya binamu yake. “Jitahidi yai” alipaza sauti. Yai lake la zambarau lilipasuka vipande. Kwenye ganda lililovunjika, kulikuwa na picha ya familia yake.
Lydia alitabasamu alipokuwa akitazama picha. Hakujali kuwa ameshindwa kwenye mchezo. Hisia nzuri, zai furaha ziliujaza moyo wakei. Alikuwa amefanya kazi kwa bidii ili kujiandaa kwa Pasaka hii kwa kusaidia na kuonyesha familia yake upendo. Kwa sababu ya Kufufuka kwa Yesu, wote wataishi tena!