Marafiki Wapendwa,
Jumapili ya Matawi mwaka huu itakuwa Jumapili ya mwisho ya mwezi wa Machi. Hiyo ni siku ya kusherehekea siku ambayo Yesu aliingia Yerusalemu akiwa amebebwa na mwana-punda. Watu walimpungia kwa matawi ya mitende wakisema kwa sauti kubwa, “Hosana!” Siku chache baadaye, Yesu aliteseka na akafa kwa ajili yetu. Kisha Akafufuka! Tunatumaini kwamba utafurahia wakati huu wa kipekee kwa kukumbuka yale ambayo Baba wa Mbinguni na Yesu wametufanyia (soma Yohana 3:16). Kwa sababu Yao, sote tutaweza kuishi tena!
Kwa upendo,
Gazeti la Rafiki
P.S. Je, kurasa ngapi unaweza kuzipata zinasimulia kuhusu Yesu katika toleo hili?
Tengeneza Yako Mwenyewe
Nilijifunza jinsi Nefi alivyotengeneza mashua (Februari 2020), hivyo nilitaka kujitengenezea yangu ili nijue jinsi Nefi alivyojisikia. Ilikuwa ngumu mwanzoni, lakini nilijifunza kutokata tamaa na kumtegemea Mungu kama alivyofanya Nefi.
Ian D., miaka 9, Veracruz, Meksiko
Tunaposoma Gazeti la Rafiki
Sisi tunapenda kusoma gazeti la Rafiki! Hutusaidia kutojihisi wapweke kwa sababu sisi ni waumini pekee wa Kanisa katika jiji letu. Huwa tunalisoma kwa Kijerumani na Kiholanzi kwa sababu mama yetu ametoka Uholanzi naye baba yetu ametoka Ujerumani.
Lars na Torben S., miaka 5 na 3, Lower Saxony, Ujerumani
Tunapenda Kuona Hekalu
Tunaishi karibu na Hekalu la Barranquilla Colombia na huwa tunakwenda huko kila baada ya wiki mbili. Hutusaidia kukumbuka maagano tutakayoweka na Baba wa Mbinguni.
Msingi Tawi la Puerto Colombia, Kolombia