Kutoka kwa Urais wa Kwanza
Amefufuka!
Imetoholewa kutoka “Amefufuka,” Ensign au Liahona, Aprili 2013, 4–5.
Kufufuka kwa Yesu Kristo kunatupa matumaini. Kulinipa matumaini ile siku ya majira ya joto mwaka 1969 wakati mama yangu alipoiaga dunia. Nilikuwa mwenye huzuni kwa sababu nilikuwa nimetengana naye kwa muda.
Lakini nilihisi furaha pale Roho Mtakatifu aliponiambia kuwa Ufufuko ni wa kweli. Ninaweza kupiga picha akilini jinsi itakavyokuwa kumwona mama yangu na wapendwa wengine tena siku moja.
Yesu Kristo alifufuka. Kwa sababu Yake, watoto wote wa Baba wa Mbinguni wanaozaliwa duniani watafufuka katika mwili ambao kamwe hautakufa.
Hadithi ya Pasaka
Kata kadi kisha uzibandike kwenye karatasi. Toboa matundu kisha uzifunge pamoja ukitumia uzi. Sasa unacho kitabu cha hadhithi ya Pasaka!
-
Yesu Kristo aliingia mji wa Yerusalemu akiwa amebebwa na mwana-punda. Watu walimsifia na kutandika chini matawi ya mitende. (Soma Marko 11:1–11.)
-
Yesu alikwenda hekaluni. Aliwaponya vipofu na vilema. (Soma Mathayo 21:12–14.)
-
Makuhani wenye wivu walimlipa mmoja wa mwanafunzi wa Yesu Kristo, Yuda Iskariote, vipande 30 vya fedha ili amsaliti. (Soma Mathayo 26:14–16.)
-
Siku alikula mlo wa Pasaka pamoja na wanafunzi Wake. Yesu aliwapa sakramenti ili kuwasaidia wamkumbuke Yeye. (Soma Mathayo 26:19–20, 26–28.)
-
Yesu alikwenda Gethsemane kuomba kwa Baba wa Mbinguni. Huko Alianza kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu. Watu wenye panga walikuja na kumkamata. (Soma Mathayo 26:36–50.)
-
Yesu aliteseka na kufa msalabani. Mwili wake uliwekwa kwenye kaburi lenye jiwe kubwa mbele ya mlango. (Soma Mathayo 27:27–35, 57–60.)
-
Malaika walilibingirisha jiwe. Waliwaambia Maria Magdalena na wanawake wengine kuwa Yesu alikuwa amefufuka. Yesu aliwatokea wale wanawake na wakamsujudia. (Soma Mathayo 28:1–10.)
-
Yesu aliwatokea wanafunzi Wake. Waligusa mwili Wake uliofufuka. Aliwaambia waifundishe injili Yake kwa kila mtu. Yesu Kristo alifufuka tena, hivyo nasi pia tutafufuka! (Soma Luka 24:36–43; Mathayo 28:16–20.)