Onyesha na Ueleze
Tulikwenda kanisani huko kijijini na tuliona kuku na bata! Ninamshukuru Mungu kwa kuwaumba wanyama.
Boris M., miaka 9, Corrientes, Ajentina
Tulipokuwa na kanisa nyumbani, niliifundisha familia yangu kuhusu kung’aa kama nyota. Kila mtu alitengeneza nyota kisha akaandika juu yake kuhusu jinsi anavyong’aa.
David A., miaka 8, Florida, Marekani
Ninafuata mfano wa Yesu Kristo kwa kuonyesha upendo na kuwasaidia wengine.
Marjorie C., miaka 7, Merseyside, Uingereza
Nilipobatizwa, sikujihisi mtu wa kipekee papo hapo, lakini baba yangu alinieleza kuwa siku moja nitajihisi mtu wa kipekee. Sasa ninajihisi kuwa mtu wa kipekee.
Aidan T., miaka 9, Alaska, Marekani
Wakati wa chakula cha mchana nilipata hisia kwamba nisicheze juu ya nondo wakati wa mapumziko. Nilipuuza hisia hiyo na nikacheza juu ya nondo. Nilianguka na kuvunjika mkono wangu. Ninajua Roho Mtakatifu atanipa maonyo kimya kimya.
McKade W., miaka 11, Washington, Marekani
Rafiki yangu wa karibu zaidi amepitia mengi, nilimtengenezea kitu cha kipekee wakati wa Pasaka. Nilipompelekea, nilijisikia vyema ndani kujua kuwa ninamsaidia rafiki yangu.
Layla P., miaka 10, Tasmania, Australia
Sakramenti
Tunapopokea sakramenti,
Tunamwomba Baba wa Mbinguni atusaidie kutubu.
Atusafishe tuwe safi kutokana na huzuni na dhambi,
Ili kila Jumapili tuweze kuanza upya.
Sisi hunywa maji na kula mkate,
Kisha tunamkumbuka kichwani mwetu.
Tunapaswa kumkumbuka Yesu daima.
Tunaishi kwa sababu Yeye alikufa kwa ajili yetu.
Madelyn R., miaka 9, Utah, Marekani
Sophia A., miaka 6, Paraná, Brazili
“Msikilize Yeye,” Scarlet H., miaka 7, Alberta, Kanada
“Amefufuka,” Eliza S., miaka 10, Idaho, Marekani
Ammon H., miaka 10, Idaho, Marekani
Joshua M., miaka 6, Hesse, Ujerumani