2021
Kutoathiriwa na Vyombo vya Habari
Machi 2021


Kutoathiriwa na Vyombo vya Habari

Picha
girl smiling and pointing up

Maswali ya Uchaguzi-Mwema

Je, utajuaje kilicho kizuri kutazama, kusoma na kusikiliza? Hapa ni baadhi ya maswali ya kukusaidia wewe kufanya uamuzi sahihi:

  • Je, inanisaidia kumsikia Roho Mtakatifu?

  • Je, inanisaidia kumfuata Yesu?

  • Je, ningejisikiaje kama Mwokozi angekuwa hapa nami?

Picha
boy looking at phone

Mpango wa Kuepuka

Je, unapaswa kufanya nini ukiona maudhui ambayo siyo mazuri? Weka mpango ili ujue cha kufanya!

  1. Zima simu, kompyuta, tableti au televisheni.

  2. Mweleze mzazi au mtu mzima unayemwamini kuhusu ulichoona na uombe msaada wao. Wao wanaweza kujibu maswali yako na kukusaidia.

  3. Fanya kitu chema. Unaweza kuimba wimbo wa Msingi, msomee ndugu yako au cheza nje na rafiki.

Picha
laptop showing video chat

Zingatia yaliyo Mema

Teknolojia inaweza kukusaidia kufanya mambo mengi mazuri. Je, imekusaidia kufanya mambo gani mazuri?

Hapa kuna baadhi ya vidokezo!

  • Piga gumzo na familia kupitia video.

  • Fanya historia ya familia.

  • Jifunze kitu kipya.

  • Tazama au sikiliza maudhui yanayokunya uwe na furaha.

  • Tembelea tovuti ya Rafiki .

Picha
Friend Magazine, 2021/03-04 Mar/Apr

Vielelezo na Jennifer Naalchigar

Chapisha