2022
Vioja Nyuma ya Jukwaa
Julai/Agosti 2022


Imeandikwa na Wewe

Vioja Nyuma ya Jukwaa

Picha
girl seeing kids talking by stage

Kaka yangu mdogo alikuwa mpumbavu, mwenye kufikiria sana, na huwajali wengine. Yeye ni mmojawapo wa mashabiki wangu wakubwa ninapokuwa jukwaani. Yeya pia ana mahitaji fulani maalum. Yeye ni mdogo sana kwa umri wake na anasumbuka kusoma, kuandika, kuzungumza, na wakati fulani kuwaelewa watu wengine. Yeye pia ni kiziwi,

Siku moja baada ya mazoezi, nilitembea kupanda jukwaa. Nilimsikia mtu fulani akiongea kitu kibaya kuhusu watoto wenye ulemavu. Kila mmoja alianza kufanya mzaha na kucheka kuhusu hivyo.

Nilijua hawakutaka kunihudhi, lakini nilihisi huzuni na nikakimbia kutafuta mahali pa kujificha. Nilipokuwa nimekaa katika sehemu yangu ya maficho, mtu mzima aliketi karibu nami na kuanza kuzungumza nami kuhusu mchezo. Nilianza kuhisi vyema.

Muda wa kuenda nyumbani ulipofika, nilimwambia mama yangu kilichojiri. Aliniambia ni SAWA kuondoka kutoka kwenye kitu ambacho kinanifanya kuhisi vibaya na kwamba ni SAWA kuzungumza na mtu mzima kuhusu hisia zangu.

Wakati mwingine watu hawaelewi jinsi inavyohisi kuwa na mahitaji maalum au kumjua mtu fulani mwenye mhahitaji maalum. Ninataka kuwa mfano wa upendo na ukarimu.

Kielelezo na Kristin Sorra

Chapisha