2022
Yesu Aliwalisha wenye Njaa
Julai/Agosti 2022


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Aliwalisha wenye Njaa

Picha
Jesus breaking bread for his disciples

Siku moja Yesu alikuwa akifundisha kundi la watu zaidi ya 5,000. Muda ulipokuwa umeenda sana, wanafunzi walitaka kuwatuma watu nyumbani wakale. Yesu hakutaka wao waondoke. Yeye alitaka kuwalisha. Lakini kulikuwa na mikate mitano na samaki wawili tu.

Yesu alikibariki chakula. Kisha wanafunzi wakakipitisha kote. Kila mtu alipata cha kutosha. Ilikuwa ni muujiza!

Picha
group of boys with all the socks they collected

Kundi la wavulana katika Utah, Marekani lilitengeneza mpango soksi wa kusaidia makundi ya hisani ambayo yanawahudumia watu wasio na makazi. Walitoa vipeperushi. Kisha siku chache baadaye, walikusanya soksi na fedha za kununua soksi zaidi. Waliweza kuchangia jozi 750 za soksi!

Chapisha