Matembezi ya Hekaluni
Ndani ya hekalu kuko vipi? Tazama ndani ya Hekalu la Rio de Janeiro Brazil ili kujua. Hekalu ni mahali ambapo watu hupokea ibada (matendo au sherehe takatifu ambazo hufanywa kwa mamlaka ya ukuhani, kama vile ubatizo).
Dawati la Kibali
Unapoingia hekaluni, mtu wa kujitolea atakukaribisha. Kama uko pale kubatizwa na kuthibitishwa kwa niaba ya wengine, utaonyesha karatasi yako ya kibali cha hekaluni. Inaonyesha kwamba wewe u tayari kuingia ndani ya hekaluni. Unaweza kupata kibali kutoka kwa askofu wako au rais wa tawi mwaka unapofika umri wa miaka 12.
Sehemu ya ubatizo
Ndani ya hekalu unaweza kubatizwa kwa niaba ya mababu zako na wengine waliokufa bila kubatizwa. Unaweza pia kuthibishwa kwa niaba yao ili waweze kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Chumba cha Ibada
Hapa utajifunza zaidi kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni na madhumuni Yake kwa ajili yetu hapa duniani. Siku moja unaweza kuja hapa kufanya maagano au ahadi maalum, pamoja Naye.
Chumba cha Selestia
Hiki chumba maridadi, chenye amani ni mahali pa kusali na kutafakari kuhusu mambo yaliyo muhimu zaidi katika maisha yako. Kinatukumbusha juu ya vile nyumba yetu ya mbinguni inavyoweza kuwa.
Chumba cha Kuunganisha
Katika chumba hiki, mume na mke wanaweza kufunga ndoa ya milele. Hii inaitwa kuunganishwa. Wenzi wanapiga magoti katika madhabahu ili kuunganishwa. Watoto pia wanaweza kuunganishwa kwa wazazi wao hapa ikiwa walitwaliwa au kuzaliwa kabla ya familia yao kuunganishwa.