2022
Nuru na Amani ya Hekalu
Julai/Agosti 2022


Kutoka Urais wa Kwanza

Nuru na Amani ya Hekalu

Imetoholewa kutoka “Napenda Kuona Hekalu,” Liahona, Mei 2021, 28–31.

Picha
President Eyring and his daughter outside temple

Kuona hekalu au picha ya mojawapo kunaweza kukupa hamu ya kwenda ndani yake siku moja. Siku itafika wakati utakapoweza kupata kibali cha hekaluni ili kufanya ubatizo hekaluni. Wakati unapobatizwa kwa niaba ya mtu aliyefariki, unamsaidia Mwokozi katika kazi yake takatifu ya kumbariki mtoto wa Baba yetu wa Mbinguni.

Miaka kadhaa iliyopita, nilienda na binti yangu hekaluni. Alikuwa wa mwisho kubatizwa siku hiyo. Mhudumu wa hekalu alimuuliza binti yangu kama angebaki kwa muda zaidi ili kubatizwa kwa niaba ya kila mtu ambaye jina lake likuwa tayari kwa siku hiyo. Alisema ndiyo.

Nilimtazama binti yangu akiingia katika kisima cha ubatizo. Ubatizo ulianza. Maji yalitiririka usoni mwake kila mara alipoinuliwa kutoka kwenye maji. Aliulizwa tena na tena, “Unaweza kufanya zaidi?” Kila mara alisema ndiyo kwa sauti thabiti. Alibakia mpaka mtu wa mwisho kwenye orodha alipokuwa amebatizwa katika jina la Yesu Kristo.

Bado nakumbuka hisia ya nuru na amani tulipokuwa tunatembea pamoja kutoka hekaluni. Hivyo ndivyo ambavyo huduma ya hekaluni hutuinua na kutubadilisha.

Nuru ya Hekaluni

Picha
temple pictures to cut out

Weka picha hizi katika nyumba yenu ili kukukumbusha kwamba unaweza kwenda ndani ya hekalu siku moja.

Vielelezo na David Habben

Chapisha