2022
Wanawake katika Agano la Kale
Julai/Agosti 2022


Kitu cha kufurahisha

Wanawake katika Agano la Kale

illustration of different women from the Bible

Oanisha kila jina na maelezo sahihi.

  1. Nilikuwa mwanamke wa kwanza duniani. Mume wangu ni Adamu Tuliishi katika Bustani ya Edeni. (Ona Mwanzo 3:20.)

  2. Mwanamume aliniomba maji kutoka kisimani. Nilimpa yeye maji na ngamia wake 10. Kisha nilienda naye kukutana na mtu aliyeitwa Isaka. Isaka akawa mume wangu. (Ona Mwanzo 24:15–19. 64–67.)

  3. Watu wangu walikuwa katika shida. Niliwaomba wasali na kufunga kwa ajili yangu. Kisha nilimuomba mume wangu, mfalme, awaokoe. Alinisikiliza, na watu wangu waliokolewa. (Ona Esta 7:2–4.)

  4. Nisingeweza kupata watoto kwa miaka mingi. Bwana aliahidi kwamba ningepata mwana. Nilikuwa na imani na subira. Bwana alinibariki kwa mwana aliyeitwa Isaka. (Ona Mwanzo 21:1–3.)

  5. Nilikuwa mwamuzi na nabii wa kike. Niliwasaidia Waisraeli kumkaribia Mungu. Niliimba wimbo kumsifu Mungu baada ya Yeye kuwasaidia watu. (Ona Waamuzi 4:4; 5:1–2

  6. Wakati mwana wangu alipokufa, mke wake, Ruthu, alinitunza. Wakati Ruthu alipoolewa tena na kupata mtoto, nilimsaidia kumtuza mwanawe. (Ona Ruthu 1:8, 14–18.)

  1. Rebeka

  2. Esta

  3. Debora

  4. Naomi

  5. Sara

  6. Hawa

Kielelezo na Simini Blocker