2022
Lengo Zuri Sana
Julai/Agosti 2022


Lengo Zuri Sana

David alikuwa na shauku ya kwenda katika Hekalu la Dubai siku moja.

Picha
boy stacking sugar cubes to make a temple model

David alifinya kiasi cha gundi kuwa vibonge vya sukari. Kisha kwa makini anaviweka katika sehemu yake.

“Wee!” Mama alisema. “Hekalu lako la vibonge vya sukari linaonekana maridadi.”

“Asante.” David alisema. “Ni Hekalu la Dubai. Nina shauku kwa ajili ya lile halisi kuwa tayari.”

David alikuwa amesisimka tangu Rais Nelson alipotangaza hekalu jipya katika nchi aliyoishi David. Muungano wa Falme za Kiarabu una baadhi ya majengo marefu duniani. Lakini haukuwa na hekalu—bado. Hili litakuwa hekalu la kwanza katika Mashariki ya Kati yote.

David alikweka kibonge cha sukari cha mwisho kwenye hekalu lake. “Ona!” alisema. “Limekamilika,”

Mama akainamisha kichwa kutazama vizuri. “Kazi nzuri! Tunapaswa kuliweka wapi?

David aliwaza. “Je, chumbani mwangu? Karibu na magari moshi yangu.” David alipenda magari moshi. Alitaka kuwa mhandisi wa gari moshi siku moja.

“Wazo zuri,” Mama alisema.

David kwa makini alibeba hekalu lake la vibonge vya sukari hadi chumbani kwake. Taratibu aliliweka karibu na mifano ya magari moshi yake. Alikuwa na shauku kuwaonyesha dada zake na baba yake.

Siku iliyofuata, Ana shangazi wa David akaja kuwatembelea. Walizungumza kuhusu mambo mengi aliyoyatazamia sana. Kisha aliwaza kuhusu kitu fulani.

“Je, unataka kujua kile kinachonipa shauku sana?”David alisema.

“Bila shaka!” Shangazi Ana alisema

“Kanisa ambalo familia yangu inahudhuria linajenga hekalu Dubai!”

Shangazi Ana alitabasamu. “Hiyo inaonekana kuwa maalum hasa.”

“Ndio!” David alisema. “Sasa hivi, hakuna hekalu la kanisa letu karibu, kwa hiyo tunaenda hekaluni Uswizi au Ujerumani. Nina furaha kutakuwa na moja karibu nasi. Nimeweka lengo la kujiandaa kwenda huko.”

“Inachangamsha jinsi gani!” Shangazi Ana alisema “Je, unafanya nini ili kujiandaa?”

“Nitasali na kusoma maandiko,” David alisema. “Na ninajaribu kumfuata Yesu Kristo. Na kisha nitakuwa tayari kwenda hekaluni!”

“Ni vyema,” Shangazi Ana alisema. “Nina hakika utafanya bidii kufikia malengo yako.”

“Nitafanya hivyo!” David aliitikia kwa furaha. Ilileta hisia nzuri kushiriki kitu fulani muhimu sana kwake.

Usiku ule, David aliomba kama angehamishia hekalu lake la vibonge vya sukari jikoni.

“Ninataka kuliweka pale tunapoweza kuliona kila wakati. Ninataka kukumbuka kujiweka tayari kwa ajili ya hekalu.”

“Hilo ni wazo zuri sana,” Baba alisema. “Nadhani kuona hekalu lako kila siku kutanisaidia mimi pia.”

Baba alimsaidia David kuhamisha hekalu la vibonge vya sukari hadi jikoni.

“Linaonekana vizuri,” Kaitlynn dada yake David alisema.

“Wakati Hekalu halisi la Dubai litakapokuwa tayari, je, naweza kuwaalika marafiki zangu waje kuliona?” David alisema.

Mama alikubali kwa kichwa. “Hilo ni wazo zuri sana.”

“Na Shangazi Ana?”

“Bila shaka,” alisema Baba.

David alitabasamu. Yeye tayari alikuwa na shukrani sana kwa ajili ya Hekalu la Dubai!

Vielelezo na Mark Robison

Chapisha