Halo kutoka Kambodia!
Ungana na Margo na Paolo wanaposafiri kuzunguka ulimwengu ili kujifunza kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni.
Kambodia ni nchi katika Asia Kusini Mashariki. Ina zaidi ya watu milioni 15.
Kuelea Taratibu
Watu wanatumia mashua zinazoitwa sampans kusafiri ndani ya mito na maziwa.
Marafiki wa Imani Zingine
Zaidi ya asilimia 95 ya watu katika Kambodia wanafuata dini ya Kibudha. Hawa watawa wa Kibudha huvaa majoho ya njano ili kuonyesha imani yao.
Lugha Moja Rasmi
Hili ndilo jina la Kanisa kwa Kikhmer, lugha rasmi ya Kambodia
Msaidizi wa Mavuno
Wali ni mojawapo ya chakula muhimu cha Kambodia. Msichana huyu anasaidia kuvuna mchele katika uwanda wenye maji unaoitwa padi.
Hekalu la Kwanza
Hekalu la kwanza ka Kambodia lilitangazwa mnamo Okotoba 2018. Waumini wa Kanisa huko walikuwa na furaha sana!