Wimbo Pendwa wa Fatima
Fatima alirukaruka mtaani. Alikuwa akitembea kwenda nyumbani kutoka shuleni pamoja na Mama. Aliimba kwa mvumo huku akirukaruka.
“Bi. Lopez alituomba tujifunze wimbo,” Fatima alisema. “Unaweza kunifundisha mmoja?”
Mama alitabasamu. “Bila shaka!”
Walipofika nyumbani, Mama na Fatima waliimba nyimbo pamoja. Waliimba nyimbo nyingi. Lakini walikuwa hawajaimba wimbo wake pendwa.
“Je ninaweza kuimba wimbo wa Msingi? Fatima aliuliza.
“Hakika,” Mama alisema.
Fatima aliimba “Families Can Be Together Forever.” Alifanya mazoezi ya maneno pamoja na Mama. Kisha aliuimba peke yake. Aliuimba mpaka akayapatia maneno yote sahihi.
Shuleni, Fatima alikuwa na shauku ya kushiriki wimbo kwenye darasa lake.
“Je, kuna mtu anayetaka kushiriki wimbo wake?” Bi. Lopez alisema.
Fatima aliinua mkono wake. “Nitaimba!”
Alisimama na kutabasamu. “Nina familia hapa duniani. Ni wazuri sana kwangu,” aliimba.
Wakati akiimba, Fatima alihisi furaha. Na alikumbuka wimbo wote! Kila mmoja darasani alipiga makofi.
Baada ya darasa, Mama alikuja kumchukua Fatima. Bi. Lopez alizumgumza na Mama.
“Aliimba wimbo mzuri, Na hakuonekana kuogopa hata kidogo.”
Fatima alitabasamu. Vivyo hivyo Mama pia.
“Tunaimba nyimbo nzuri kila wiki kanisani!” Fatima alisema.
“Unaweza kuja nasi wakati wowote,” Mama alisema.
Bi. Lopez alitabasamu. “Asante.”
Fatima aliimba alipokuwa akitembea kwenda nyumbani na Mama. Alipenda kushiriki wimbo kwenye darasa lake. Kuimba kulimfanya ahisi furaha.