2022
Eliya na Sauti Ndogo Tulivu
Julai/Agosti 2022


Hadithi za Maandiko

Eliya na Sauti Ndogo Tulivu

Picha
Elijah walking up a mountain

Eliya alikuwa nabii. Alitaka kuisikia sauti ya Mungu. Alienda mlimani ili kuisikia sauti ya Mungu vyema.

Picha
Elijah watching rocks and trees blow

Kulikuwa na upepo mkali. Ulikuwa mkali sana hata ukavunja miamba. Upepo ulivuma kwa sauti kubwa. Lakini haikuwa sauti ya Mungu.

Picha
flames from a fire

Kisha pakawa na tetemeko la ardhi. Nchi ilitikisika. Kulikuwa na moto pia. Ulikuwa na miale mikubwa. Lakini tetemeko na moto havikuwa sauti ya Mungu.

Picha
Elijah watching a peaceful sunset

Kisha kukatulia. Eliya akaisikia sauti ya Mungu. Ilikuwa ndogo na tulivu. Lakini ilikuwa dhahiri.

Picha
children sitting in sacrament meeting

Ninaweza kuisikia sauti ya Mungu kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu. Yeye huongea nami kwa njia ndogo ndogo na rahisi.

Chapisha