Mikono ya Usaidizi Ulimwenguni Kote
Kutana na Septream kutoka Kambodia
Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.
Yote kuhusu Septream
Umri: miaka 12
Kutoka: Phnom Penh, Kambodia
Lugha: Kikhmer, Kingereza
Malengo na ndoto: 1) Kuisaidia Kambodia kuwa nchi bora nitakapokua. 2) Kutumikia misheni. 3) Kwenda hekaluni.
Familia: Septream, Mama, Baba, dada wawili, kaka mmoja
Mikono Saidizi ya Septream
Septream huenda shuleni katika mji mkubwa. Wakati mwingine huko shuleni yeye huwatambua marafiki ambao hawana chakula cha kutosha. Kwa hiyo yeye hushiriki vitafunwa na chakula pamoja nao. Septream husema kuwasaidia wengine humfanya kuhisi vizuri. “Kunanifanya nitake kufanya hivyo zaidi. Ninahisi furaha ninapomfuata Yesu,” yeye husema.
Septream husema tunabarikiwa tunapowatumikia wengine. “Tunapofanya jambo zuri, Mungu atatubariki. Yesu husema kwamba kufanya mambo mazuri kwa wengine ni kama kumfanyia Yeye mambo mazuri.”
Vitu Pendwa vya Septream
Hadithi kuhusu Yesu: Wakati alipomsaidia Petro kutembea juu ya maji.
Mahali: Nyumbani
Wimbo wa Msingi: “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3)
Chakula: Amok (samaki aliyepikwa katika majani ya ndizi)
Rangi: Samawati
Masomo Shuleni: Kingereza na historia