2022
Shule Mpya, Rafiki Mpya
Julai/Agosti 2022


Shule Mpya, Rafiki Mpya

Je, Ada angeweza vipi kupata marafiki ilhali hakuweza kuongea Kichina?

Mom hugging young girl wearing backpack

“Mie naogopa,” Ada alisema. Ilikuwa ni siku yake ya kwanza shuleni nchini Taiwan. Lakini hakuongea Kichina kama wanafunzi wengine. “Angewezaje kupata marafiki? Ni nani angecheza naye wakati wa mapumziko?

Mama alimpa Ada kumbatio kubwa. “Ni SAWA kuwa na uoga.”

Ada alikunja uso. “Sijui jinsi ya kupata marafiki hapa.”

Mama alimpa kumbatio lingine. “Ikiwa una wasiwasi, pengine unaweza kufikiria wimbo wa Msingi. “Je, hiyo itasaidia?”

Ada aliitikia kwa kichwa. Kisha alitembea na Mama yake kwenda darasani. Mwalimu wake alikuwa akimsubiri. “Ni hao!” mwalimu alisema. Ada alijaribu kutabasamu. Hakujua kile ambacho maneno hayo yalimaanisha.

Ada alisema kwaheri kwa Mama. Kisha alitafuta dawati na kuketi.

Aliwaangalia watoto wengine. Baadhi yao walikuwa wakiongea wao kwa wao. Wengine walikaa kimya kama Ada. Ada alikuwa na wasiwasi. Alihisi kama nyuki walikuwa wakivuma tumboni mwake.

Kisha Ada alimwona msichana analia. Ada alitaka kumsaidia. Lakini ni kwa jinsi gani angeweza kusaidia wakati hazungumzi Kichina? Vipi ikiwa msichana hakutaka usaidizi?

Lakini kisha Ada akafanya kile Mama alichosema. Alifikiria maneno ya wimbo wake pendwa wa Msingi: “Pendaneni kama Yesu anavyowapenda.” Ada alijua Roho Mtakatifu alikuwa akimwomba asaidie.

girl comforting other child who is crying

Ada alikaa karibu na msichana. Akamkumbatia kwa mikono. Kisha akampigapiga mgongoni kama vile Mama alivyomfanyia Ada wakati alipokuwa na huzuni. Msichana aliacha kulia! Alimkumbatia Ada.

Ada akajionyoshea kidole. “Ada.”

Msichana akajinyoshea kidole. “Mei,” alisema.

Ada alitabasamu. Aliketi karibu na Mei wakati wote wa siku. Hata ingawa hawakuongea lugha moja, walifurahia pamoja. Walikula chakula pamoja. Walicheza pamoja wakati wa mapumziko. Na Mei alimsaidia Ada kujifunza maneno mapya ya Kichina!

two girls jumping rope together

Ada alikuwa na shauku ya kumwambia Mama kuhusu rafiki yake mpya. Alijua kwamba kama angemfuata Yesu, hangekuwa na haja ya kuogopa.

Vielelezo na Shawna J. C. Tenney