Kumfuata Yesu kwa Pamoja
Zach W., umri miaka 8, Ohio, Marekani
“Sali Kila Siku,” Amelia S., umri miaka 8, Andhra Pradesh, India
“Pasaka ya Yesu,” Indira G., umri miaka 9, Lower Saxony, Ujerumani
Nora na Moses B., umri miaka 7 na 9, Amman, Jordan
Taggart W., umri miaka 10, Utah, Marekani
“Watoto Watangulizi Waliimba Walipokuwa Wakitembea,” Emily J., umri miaka 10, Utah, Marekani
Nilianza kusoma Kitabu cha Mormoni nilipofikia miaka saba ili kujiandaa kwa ajili ya ubatizo wangu. Nilikimaliza kwenye siku yangu ya mwaka wa nane wa kuzaliwa! Kulikuwa na maneno magumu lakini hadithi nyingi za kuvutia.
Heewon C., umri miaka 8, Gyeonggi-do, Korea ya Kusini
Daima ninasoma Kitabu cha Mormoni. Sehemu yangu pendwa ni hadithi ya Nefi.
Jared C., umri miaka 6, Sololá, Guatemala
Tulienda kwenye mazingira ya hekalu. Ilinifanya nisisimke kwa furaha kufanya ubatizo hekaluni nitakapofika umri wa kutosha. Nilihisi furaha nilipokuwa huko. Hekalu ni zuri sana.
Emmeline M., umri miaka 10, New Jersey, Marekani
Ninaposali na kusoma maandiko kila siku, ninahisi kuwa karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Rafael L., umri miaka 8, Arequipa, Peru
Baadhi ya michezo yangu ya besiboli inakuwa Jumapili. Nina huzuni siwezi kwenda kwenye yote lakini nina furaha ninaweza kwenda Kanisani. Daima ninataka kuwa katika mahali sahihi katika siku ya Sabato.
Benjamin P., umri miaka 7, New York, Marekani
Mama yangu alisema ninaweza kupata mtambaazi kama nikipata fedha. Ilichukua muda kwa sababu nililipa zaka. Wakati tundu la mtaambazi lilipokuwa linauzwa, nilikuwa na fedha ya kutosha kulinunua. Siku iliyofuata nilipata kinyonga wangu kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa. Hii ilinisaidia kupata ushuhuda wangu juu ya zaka.
Laura K., umri miaka 11, Minnesota, Marekani