Ina Maana Gani Kukusanya Israeli? Rafiki, Septemba 2024, 22.
Kadi za Mahekalu
Ina Maana Gani Kukusanya Israeli?
Kukusanya Israeli inamaanisha kusaidia watu kufanya na kuweka maagano, au ahadi, na Baba wa Mbinguni. Ndani ya Hekalu tunaweza kufanya hivi kwa kubatizwa kwa niaba ya wale waliofariki. Manabii wameahidi kwamba tunaposaidia kukusanya Israeli, tunahisi upendo wa Yesu Kristo kwa ajili yetu.
Harare Zimbabwe
-
Hili litakuwa hekalu la kwanza huko Zimbabwe.
-
Mzee Edward Dube, ambaye ni wa kutoka Zimbabwe, alitoa sala wakati wa kubariki ardhi. Alisali kwamba hekalu litasaidia kugeuza mioyo ya watu kwa Yesu Kristo.
Freiberg Ujerumani
-
Hekalu hili lina kuta za matofali ambayo yana unene wa futi 2 (cm 60).
-
Lilipokamilika mnamo mwaka 1985 lilikuwa hekalu dogo mno kuliko yote.
-
Takribani watu 90,000 walihudhuria katika wiki mbili za ufunguzi wake.