Rafiki
Mazungumzo na Teancum kuhusu Maandiko
Septemba 2024


“Mazungumzo na Teancum kuhusu Maandiko,” Rafiki, Septemba 2024, 40–41.

Mazungumzo na Teancum kuhusu Maandiko

Teancum anatoka Fiji. Tulimuuliza maswali kadhaa kuhusu jinsi anavyojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni.

Tuambie kuhusu wewe mwenyewe.

Teancum

Nina umri wa miaka 9 na mdogo kati ya watoto sita. Rangi niipendayo ni rangi nyekundu, na chakula nikipendacho ni kuku wa viungo na wali. Ninapenda kucheza ragbi! Kitu cha ajabu kuhusu mimi ni jina langu. Jina langu la kwanza ni kutoka shujaa wa Kitabu cha Mormoni, jina langu la pili ni kutoka mjomba wangu wa Nigeria, na jina langu la mwisho ni la Kifiji.

mvulana akicheza mpira wa rugbi
Kuku wa viungo na wali

Nini kinakusaidia kujifunza kutoka kwenye maandiko?

Familia ikisoma maandiko

Ninapenda kusoma maandiko pamoja na familia yangu. Tunajifunza kutoka kwenye masomo ya Njoo, Unifuate pamoja. Napenda kujifunza hadithi mpya kila wiki. Tunazungumza kuhusu kile tunachojifunza na kushiriki ushuhuda wetu sisi kwa sisi. Wakati ninaposoma maandiko, pia ninapenda kujifikiria mwenyewe katika hadithi hizo.

Ni kwa jinsi gani maandiko yanakusaidia?

Mvulana akisali

Maandiko yananikumbusha kuwa shupavu na jasiri na kusali kwa ajili ya faraja. Wakati wowote ninapoogopa au kuwa mpweke, ninajua Roho Mtakatifu daima atanifariji.

Ni hadithi gani ya Kitabu cha Momoni unayoipenda?

Teankumu katika maandiko

Hadithi ninayoipenda kutoka katika Kitabu cha Mormoni, ni hadithi kuhusu Teankumu kwa sababu alikuwa kiongozi mkubwa na shujaa. Alipigana kwa ajili ya familia yake, rafiki zake na Kanisa. Ninajua ninaweza kuwa kama yeye pia na daima kulinda kile ninachokipenda sana.

Ni ushauri upi ungempa mtu ambaye amekuwa na muda mgumu kuelewa maandiko?

Kama mtu fulani anahangaika kujifunza kutoka kwenye maandiko, wanaweza kuwaomba mama au baba zao au hata ndugu zao kuwasaidia. Familia yangu kwa kweli hunisaidia. Ungeweza pia kumuuliza mwalimu wa Darasa la Watoto au kiongozi kanisani!

PDF

Vielelezo na Augusto Zambonato