2023
Wapendwa wa Mungu
Septemba 2023


Wapendwa wa Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Sept. 2023.

Njoo, Unifuate

1 Wakorintho 11

Wapendwa wa Mungu

Katika mpango wa Mungu wa furaha, kila msichana na mvulana ana azma tukufu, kila mmoja wenu anapendwa na anahitajika.

Mzee Gong akiwa na vijana

Fikiria jinsi ambavyo muziki ungekuwa kama kila chombo kingetoa sauti ileile. Ingekuwaje kama kila nota ya piano ingetoa tuni ileile au kama kila sauti kwenye kwaya zingefanana? Hii ingefanya muziki uchoshe sana!

Kwa furaha, sauti za ala za muziki na kwaya zinatofautiana katika sauti na tuni. Nota kutoka upande mmoja mpaka wa pili wa piano zinatoa sauti tamu nyingi, na kwaya zinatoa ulinganifu wa sauti mzuri. French horns, tuba, violini, na ngoma, kila moja inaongeza sauti ya kipekee kwenye ulinganifu wa sauti wa okestra.

Uimara na Karama

Kama ilivyo kwa muziki, Baba wa Mbinguni anafurahia katika talanta tofauti tofauti, nafsi mbalimbali, na uzoefu wa kila mmoja wa watoto Wake, kila mwana na binti mpendwa. Kwa hali yako yoyote, maisha yako kokote miongoni mwa mataifa, koo na watu, Baba wa Mbinguni anashangilia ukuaji wako usio na kikomo, vile unavyoweza kuwa, kupitia utii, rehema na upendo.

mvulana akipiga kinanda

Kwa upendo mkuu, Anakualika wewe ugundue utambulisho wako mtukufu na ukamilishe azma yako tukufu. Anakutia moyo uendeleze karama zako za kiroho, tabia ya kiungu, na uwezekano wako mkubwa mno. Na Anakupa fursa za kila siku za kujifunza namna ya kuwaona na kuwahudumia wale wanaokuzunguka kama Yesu Kristo ambavyo angefanya.

Katika mpango mtukufu wa Mungu, tunakuja kwenye ulimwengu huu kupitia mama na baba. Familia huwahitaji wote wawili. Pamoja, kama wenzi walio sawa, wazazi wanazitunza na kuzihudumia familia zao. Katika nyumba zetu, akina baba na waume wanatakiwa kuongoza kwa upole, unyenyekevu, na upendo wa kweli—sifa takatifu ambayo wanaume na wanawake tunaihitaji kwenye mahusiano yetu yote. Mbingu husikitika pale, katika mahusiano yoyote kukiwa na unyanyasaji, udikteta, au ulazimishaji wa aina yoyote, kutoka kwa wanaume au wanawake. Ushawishi, ustahimilivu, huruma, na elimu safi ni sifa kama za Kristo ambazo kila mmoja wetu anazitafuta.

Bila shaka, hakuna aliye mkamilifu—hata familia yoyote. Bila kujali hali yako, waheshimu wazazi wako na ipende familia yako—familia uliyonayo na familia ambayo siku moja utakuwa nayo. Mwokozi wetu anaweza kukusaidia uelewe, usamehe, na uwatie moyo wale wanaokuzunguka. Unapofanya kwa juhudi zako zote, Bwana atakusaidia na kukuongoza. Tafadhali kumbuka msimamo wako mbele za Bwana na kwenye Kanisa lake huamuliwa kupitia tabia zako binafsi na uadilifu katika kushika maagano yako na Mungu.

sakramenti

Ukuhani na Mpango wa Mungu

Mungu anatupenda zaidi na anatujua vyema kuliko tunavyojipenda au kujijua. Mamlaka yake ya ukuhani yametolewa kubariki watoto Wake wote. Akina kaka wastahiki wanashikilia ukuhani, lakini wao siyo ukuhani. Rais Russell M. Nelson anafundisha kwamba ukuhani “ni muhimu kwa [wanawake] kama vile ilivyo kwa mwanamume yeyote.” Ukuhani unawapa wanawake na wanaume “njia ya kufikia kwenye…hazina zote za kiroho Bwana alizonazo kwa ajili ya watoto Wake.”1

Wavulana na wasichana kwenye kompyuta

Kuhudumu Pamoja

Katika Kanisa la Bwana, tunashauriana katika baraza tunapohudumu pamoja. Katika mabaraza yetu, viongozi wanatafuta utambuzi na mawazo kutoka kwa wote, ikijumuisha wasichana na wavulana. Katika kila jambo, tunafikia maamuzi mazuri na kuwa na ufanisi mkubwa mno katika huduma ya Bwana pale tunapothamini mchango wa mwingine na kufanya kazi pamoja, akina kaka na akina dada katika kazi Yake.

Katika kata zetu na matawi, wavulana na wasichana wanaongoza madarasa na akidi. Katika baraza la vijana la kata, viongozi wetu wa vijana kwa pamoja wanamsaidia kila kijana kuunganika na mbingu, viongozi wetu wa Kanisa, na vijana wengine. Kama wahudumiaji wenza kwa watu wazima, wavulana na wasichana wetu huwafikia na kuwabariki wengi. Katika huduma yetu, sisi sote husimama pamoja.

Wavulana na wasichana wakihudumu pamoja

Ni baraka iliyoje kwamba wavulana na wasichana huudumu kama mashahidi wa ibada za injili ya urejesho. Ninyi ni mashahidi kwenye ubatizo wa wote walio hai na ubatizo kwa niaba ya mababu hekaluni. Mnahudumu pia katika sehemu zingine kwenye nyumba ya Bwana.

Baraka za Agano na Mungu

Binafsi, kila msichana na kila mvulana anafanya maagano matakatifu na Mungu. Wakati kwa imani yanapoheshimiwa, maagano yetu na Mungu yanaleta baraka Zake—kubwa mno kuliko tunavyoweza kufikiria. Maagano yetu na Mungu yanaweza kutakasa matamanio na matendo yetu. Maagano yetu na Upatanisho wa Kristo vinaweza kutusaidia tuwe kama mtoto wa Mungu—myenyekevu, mstahimilivu, aliyejaa upendo (ona Mosiah 3:19). Katika vyote tunavyofanya, tunaanza na Yesu Kristo. Tunamchagua Yeye kwanza miongoni mwa chaguzi zetu nyingi, na tunamweka Yeye kwanza katika kila uchaguzi tunaoufanya.

Yesu Kristo

Mtumainie Mwokozi

Unaweza kupata uzoefu wa furaha, hisia za upendo katika moyo wako pale unapomweka Yesu Kristo katika kiini cha mafunzo yako ya injili, huduma, shughuli na maendeleo binafsi na unapochagua mema. Juhudi zako zenye kiini kwa Kristo zinaweza kuwa burudani na thawabu unapowasaidia wengine kwa huruma na upendo wa kweli.

Mambo ya makuu hutokea wakati vijana wa kiume na wa kike wanapompenda Bwana na kutumikia pamoja kwa umoja na upatano. Hii ni kweli kwenye seminari, shughula za kawaida za vijana, na KNV.

msichana

Kwa upendo usio na kikomo, Baba yetu wa Mbinguni anamwalika kila msichana na mvulana “na anawakaribisha wote kuja kwake na kupokea wema wake; na hamkatazi yeyote anayemjia”.(2 Nefi 26:33).

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanakupenda. Watakusaidia na kukubariki uwe mwenye furaha ya kweli. Tafadhali mchague Mwokozi wetu Yesu Kristo kwanza. Mwamini Mungu na uwe na umoja katika Yesu Kristo pamoja na wote wanaokuzunguka. Kama mtoto mpendwa wa Mungu, unaweza kujiunga na kuwa wa jamii ya Watakatifu ambayo ni Kanisa Lake lililorejeshwa—Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Jinsi ulivyo na jinsi utakavyokuwa vinahitajika katika ulimwengu wa leo. Ni utofauti kiasi gani unaoweza kuleta kwenye familia yako, katika Kanisa Lake lililorejeshwa, na katika ulimwengu.

Katika Yesu Kristo, vitu vyote vizuri vinawezekana. Katika Yesu Kristo, vitu vyote vya kweli vitafanyika, katika muda wa Mungu na katika njia Yake. Kama mmoja wa mashahidi Wake maalumu, Nina shuhudia na kuahidi.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho,” Okt. 2019 mkutano mkuu (Ensign au Liahona,, Nov. 2019, 77).