2023
Kondoo Aliyepotea
Septemba 2023


“Kondoo aliyepotea,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2023.

Mifano ya Mwokozi

Kondoo Aliyepotea

(Luka 15:4–7)

Picha
Bango: Kondoo Aliyepotea

Pakua PDF

Mchungaji mwema alikuwa na kondoo 100. Mmoja akawa amepotea.

Aliwaacha 99 ili kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea.

Na alikuwa na furaha wakati alipompata kondoo. Alimbeba mabegani mwake mpaka nyumbani, akishangilia.

Aliwaita rafiki zake na majirani. “Furahini pamoja Nami,” alisema, “kwa kuwa Nimempata Kondoo wangu aliyepotea” (Luka 15:6).

Ina maana gani?

Wale wanaotenda dhambi ni kama kondoo waliopotea. Mwokozi alifundisha kwamba kuna furaha mbinguni wakati mwenye dhambi mmoja anapotubu (ona Luka 15:7).

Chapisha